Lete hoja au swali lolote kuhusu CCM ujibiwe hapa

Lete hoja au swali lolote kuhusu CCM ujibiwe hapa

Habari zenu watanzania!

Huu ni mwaka wa uchaguzi ambapo zimebaki miezi michache chama chetu pendwa ccm kwenda kujinyakulia ushindi wake wa kishindo kuanzia kuanzia ngazi ya za chini kabisa hadi urais...


Jitokezeni kwa wingi kusapoti chama chenye uhakika wa kushinda ili mpendwa wetu Jpm aendelee kulinyoosha taifa.
1) Ile 1.5 trillion ambayo haikujulikana matumizi yake kwa mujibu wa ukaguzi wa CAG, mnatumbiaje leo?
2) Wale wafungwa pale Dodoma kupandisha bendera zenu, hii imekaaje au ndo matumizi mabaya ya madaraka?
3) Kuondolewa kwa bunge live mlituambia ni kupunguza gharama na kwamba Wananchi hawana muda wa kuangalia kwani wanakuwa kazini tupeni tathimini leo maana wengi tunajua hoja hizi zilikuwa ni hadaa tu za kuwaongopea watz ili mtimize malengo yenu
4) Deni la Taifa leo ni kiasi gani ukilinganisha na kipindi kilichopita?
5)TBC inahudumiwa na ccm au serikali?
6) CCM wamefanya siasa peke yao kwa miaka 5, nini kinawafanya leo waogope upinzani kiasi hicho?
7) Je ni nini tathmini yenu, kwa kadri ya malengo yenu ya kufuta upinzani ifikapo 2020?
 
Mwalimu Nyerere baba wa Taifa alituambia, ili tuendelee tunahitaji..

Siasa safi.
Uongozi bora.
Watu.

Taifa la Tanzania lina watu zaidi ya 50milioni na ardhi kubwa sana, kwa hiyo watu sio tatizo..

TATIZO NI NINI SASA MPAKA TUKO HAPA?
 
Habari zenu watanzania!

Huu ni mwaka wa uchaguzi ambapo zimebaki miezi michache chama chetu pendwa ccm kwenda kujinyakulia ushindi wake wa kishindo kuanzia kuanzia ngazi ya za chini kabisa hadi urais...


Jitokezeni kwa wingi kusapoti chama chenye uhakika wa kushinda ili mpendwa wetu Jpm aendelee kulinyoosha taifa.
CCM maana yake nini?
 
Sasa wewe unaharibu mjadala! Video clips zipo kuanzia za Ma-DC hadi Mwenyekiti wako na most recent akiwa kwenye jumbo la Mheshimiwa Bwege aliongea pia ina akiwa Morogoro aliongea hadi akaambiwa kuwa ni jimbo linaloongozwa na CCM. Brother usitufanye wote vilaza
Hizo kauli hazimaanishi kwamba maendeleo hayatafika maeneo yenye wapinzani, kwa mfano mpinzani anaweza kusema, "Ccm tangu uhuru hadi sasa haijafanya maendeleo yoyote" we unaona ni kweli kauli hiyo? Kwa hiyo kuna muda ambapo viongozi wa ccm au vyama vingine huwa wanaongea maneno ya kuwavuta watu waende kwenye vyama vyao ila sio kila kinachosemwa ndo kilivyo.
 
Takwimu hiyo umeipata wapi ndugu?

Karibu sana ccm chama tawala.

Sasa ulitegemea takwimu kama hizo nitazipata NBS kweli?.. Jibu swali, usiulize swali. Kwanini wapiga kura wengi wa CCM ni watu wasiokuwa na elimu na uwezo mkubwa wa kupambanua hali halisi ya uchumi wa watu na wa nchi??..
 
Kuna maendeleo makubwa yamefanywa zaidi ya hizo laptop na million50 kwa kila kijiji...

Karibu ccm ndugu chama tulivu.
Nashauri usiwe mpiga debe wa mgombea yeyote.

Maana majibu yako hayana uwezo wa kubadilisha misimamo ya wajumbe.
 
Hizo kauli hazimaanishi kwamba maendeleo hayatafika maeneo yenye wapinzani, kwa mfano mpinzani anaweza kusema, "Ccm tangu uhuru hadi sasa haijafanya maendeleo yoyote" we unaona ni kweli kauli hiyo? Kwa hiyo kuna muda ambapo viongozi wa ccm au vyama vingine huwa wanaongea maneno ya kuwavuta watu waende kwenye vyama vyao ila sio kila kinachosemwa ndo kilivyo.
Naomba nikushauri jambo, huu mjadala huuwezi na ni ngumu sana kuwatetea CCM! MÀra unakana Mara unakubali....jitahidi kuachana na kuitetea CCM utapasuka kichwa! Evidence zote zipo huko, nenda hata hapo Kibamba tu kaangalie, kisa? Walimchagua Mpinzani! Sasa wewe leo unajifanya kukataa!! Unatia hasira sana!
 
Sasa ulitegemea takwimu kama hizo nitazipata NBS kweli?.. Jibu swali, uliulize swali. Kwanini wapiga kura wengi wa CCM ni watu wasiokuwa na elimu na uwezo mkubwa wa kupambanua hali halisi ya uchumi wa watu na wa nchi??
Hoja nzuri ni kwamba unaposema wapiga kura wa ccm ni watu wasio na elimu unapaswa kuweka wazi vile umelitambua jambo hilo vinginevyo ni kwamba unaleta ubishi tu...ccm ina watu wa kila aina
 
Naomba nikushauri jambo, huu mjadala huuwezi na ni ngumu sana kuwatetea CCM! MÀra unakana Mara unakubali....jitahidi kuachana na kuitetea CCM utapasuka kichwa! Evidence zote zipo huko, nenda hata hapo Kibamba tu kaangalie, kisa? Walimchagua Mpinzani! Sasa wewe leo unajifanya kukataa!! Unatia hasira sana!
Usipate hasira ndugu, twende kidogokidogo tu tutaelewana...mambo mazuri yanahitaji mpangilio
 
Ajira zinatolewa ila sio rahisi kwa vijana wote kupata ajira, hakuna kabisa nchi inayoweza kufanya hivo...sisi tunajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu ili angalau % kubwa ya vijana wapate ajira
Lete data mkuu usiongee kama mwanasiasa.
 
Kwenye ilani ya chama cheny ya mwaka 2015 mmesema kuwa mtakamilisha mchakato wa katiba mpya uliokuwa umebakisha kura ya maoni tu. Kwa nini serikali ya chama chenu imeikana ilani yake yenyewe katika suala hilo?
 
Je kuna faida gani ya kujenga duplicate capital Dodoma na State house,huoni mmegeuka malinbukeni wa kutumia kodi zetu kwa vitu vya hovyo?
 
Sio kila jambo litakamilika kwa wakati mmoja, tunaenda kidogokidogo chagua ccm tena ili yale ambayo hayatekelezwa awamu ya 2015-20 yatekelezwe 2020-25


Karibu ccm
Hizi story mlidanganya nazo 2015 watumishi wakawapa kura alafu mmewatelekeza kwa miaka 6 alafu tena mnakuja na ahadi ile-ile mliyodanganya.
 
Kesi za uongo na kubambikizia watu ni sera za ccm? Mbili, utekaji na kudhuru wakosoaji ni sera za ccm mpya? Majibu tafadhali
 
Kwanini CCM imemrudisha kugombea mtu akiyejiita kichaa na mwenye wazimu?
 
Sio kila jambo litakamilika kwa wakati mmoja, tunaenda kidogokidogo chagua ccm tena ili yale ambayo hayatekelezwa awamu ya 2015-20 yatekelezwe 2020-25


Karibu ccm
Haa chagua CCM ili uchumi wa mtu mmoja mmoja uendelee kudidimia
 
Back
Top Bottom