Bei za bidhaa zinategemea pia na eneo bidhaa hizo zinapouzwa, mfano: Chupa 1 ya bia zinazofanana kwa kila kitu inaweza kuuzwa bei kwenye hoteli za kitalii, lakini ikauzwa kwa bei ya chini kwenye kibanda cha Mangi. Bei za bidhaa za mlimani city huwa zinajumuisha mambo mengi yanayotokana na mazingira ya mlimani city, mambo kama kodi, usalama, hustle free environment, etc.,. Kwahivyo, unaponunua bidhaa mlimani city kwa gharama ya juu, sio lazima imaanishe kwamba bidhaa hiyo ina viwango bora zaidi ya zile za kariakoo, au endapo utanunua bidhaa hiyo hiyo kariakoo kwa bei ya chini, haimaanishi kwamba bidhaa za kariakoo zina viwango hafifu. Na kwa vyovyote vile, bei za Mlimani city zinaweza zisiwe ndio bei msingi za soko.