Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Jana tarehe 01 Aprili 2025, LHRC ilipokea taarifa za kuuawa kwa mwananchi mmoja aitwae Emmanuel Lucas Mwenye umri wa miaka 18 mkazi wa Kijiji cha Kisangura Wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara kilichosababishwa na askari wa Jeshi la Magereza Sijali William Hence na Linus Mushumbusi wanaohudumu katika gereza la Tabora B lililipo wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara.
Emmanuel Lucas alifariki dunia tarehe 31 Machi 2025 baada ya kupigwa risasi na askari hao akidaiwa kuingiza mifugo katika eneo la magereza.
LHRC inazo taarifa za Jeshi la Polisi kuchukua hatua za awali ikiwemo kuwatia mbaroni watuhumiwa, hivyo LHRC inatoa wito kwa Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa haraka na kuhakikisha haki inatendeka.
Hata hivyo, tutaendelea kufuatilia kwa karibu juu ya hatua zitakazochukuliwa ikiwemo kuwafikisha watuhumiwa mahakamani haraka iwezekanavyo kwa mujibu wa Sheria.
Mwisho, LHRC inatoa wito kwa wananchi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza maeneo yaliyotengwa ili kuepusha migogoro na vifo visivyo vya lazima.
Imetolewa na LHRC