Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa taarifa ya Onyo kwa Mkuu wa Mkoa Arusha, Paul Makonda baada ya kuonekana kwenye Video akitoa kauli za udhalilishaji dhidi Mtumishi wa Kike kutoka Longido
Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dkt. Anna Henga, amesema ""Tumepokea kwa masikito Video inayomuonesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha akimdhalilisha Mtumishi wa jinsia ya Kike kule Longido. Tunakemea vikali kauli hizo hasa kwa Mtu kama yeye Mkuu wa Mkoa"
Aidha, LHRC imemtaka Makonda kuomba radhi na kuacha tabia hiyo kwasababu inatweza Utu wa Mwanamke na kushusha juhudi za kutetea Haki za Wanawake huku Viongozi kama yeye wakitoa kauli zinatoa mifano mibaya kwa watu wengine
Kupitia Video hiyo, RC Makonda anasikika akimtaka Mtumishi huyo kuzungumza vizuri na si kama anaongea na mtu anayetaka kumposa au yuko kwenye Kitchen Party na pia yeye (RC) ana Mke mzuri