Mkuu,
Kwani hata mwanamke wako si unamhudumia ili akufurahishe, mkimaliza unampa nauli, ukitaka aje kwako si unatuma nauli?
Naona wanakuwa wakali, ukweli unauma sana. They were made to make us happy!
Mkuu Eroni,
Kufanya mjumuisho wanawake kuwa ni chombo cha starehe huo ni uvunjivu wa hoja “fallacy of generalization “
Mkuu wangu Eroni,
Mpaka unafika hapo kwa kiasi kikubwa kuna uwepo wa mwanamke ambaye amepambana kwa kiasi kikubwa. Sidhani kama unaweza kupata nguvu ya kusema mwanamke huyo ni chombo cha starehe tu.
Kama unafikiri mwanamke unamuhudumia ili awe chombo cha starehe kwako ni mtazamo wako na ninauheshimu.
Fikiria ni kwa kiasi gani mama au mlezi wako yoyote wa jinsia KE alivyopambana kwa ajili ya maisha yako. Ni sawa kumuita chombo cha starehe? Sababu chombo cha starehe ni kwa ajili ya starehe na raha tu.
Hii ni mitandao na Hivi vitu kuna watoto ambao wapo kwenye early’s 18 wanapita humu atakapokutana na kauli. Kama hizi hujui zitamjenga kiasi gani.
Halafu hii sentensi “They were made to make us happy” sio sawa sababu wapo wanawake wenye pesa ambao hutumia kuwapata vijana wasiotaka kufanya kazi na kujituma hivyo ni halali kusema “ Men are made to make us happy”
Halafu sentensi “They were made to make us happy” ni sentensi uliyoitengenezea majibu yako kwamba mwanamke ameumbwa na kitu fulani ambacho hata tukikuambia uthibitishe hutaweza.
Kama unatumia kigezo cha Imani it rather to use “ were made to make happy each of us” sababu wote tunahisia, tunapenda, tunakasirika.
Kusema jinsia fulani ipo kwa ajili ya kuipa furaha jinsia fulani si kweli.
I hope your mama is very of proud of who you are today. And I hope your daughters if you have them they are very happy to have a father-figure like you.