Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hao kwanza wanapewa za uso. Ndio wanaolea wajinga wajinga kwenye jamii kwa mazindiko na uchawi waoWamo na kuna project maalum za hiyo kaliba... Kule kuna kila kitu
Siyo rahisi kupata mfano maana kazi zao ni siri.Nipe mfano mzuri....
Bado nimekwama hapa kwenye Apson... Umezidi kunivurugaApson
Rostan
mmmh bado ngumu kumesa hebu niloge Kwanza akili zinikae sawa maana daa nashindwa ng'amua code!Apson
Rostan
mkuu inabidi ndugu mshana jr atuloge kidogo maana hata Mimi akili zangu zimegoma kufungua code😂😂Bado nimekwama hapa kwenye Apson... Umezidi kunivuruga
Sukuma gang mmeanza kuweweseka[emoji23][emoji23]
Sasa it's far better to declare that at the top of your thread. Tafadhali zingatia
Mwanzo nilidhani AM ni huyu muandika riwaya mwenye urafiki na Chidi BENZI au RUKSA kukosolewa!!? Mshana Jr tunaomba hints hapa angalau tuambulie chochotemkuu inabidi ndugu mshana jr atuloge kidogo maana hata Mimi akili zangu zimegoma kufungua code[emoji23][emoji23]
Bora u-type jina lake vzr kisha ullifute comment yako ndani ya dkk moja tu kuu,Mwang'onda...
Upo slow sana jaribu fatilia wakuu wazee wa kaunda utapata jibuBado nimekwama hapa kwenye Apson... Umezidi kunivuruga
Kutoa roho ya mtu ni tofauti kabisa na kutoa roho ya mnyama ama mdudu. Kwa mnyama sana sana unaweza kulipishwa fidia hasa kama mnyama mwenyewe ni kwa ajili ya utalii.
Kutoa roho ya mtu ukiachana na ule ugomvi wa papo kwa papo kunahitaji maandalizi yake! Na wengi kwenye hayo maandalizi hukosea kitu kidogo sana na hatimaye kujulikana, kukamatwa kufunguliwa mashtaka na hatimaye kuhukumiwa kifo ama vifungo vingine! Kuachiwa huru ni aghalabu!
Kwa kuzingatia hili kuna kaliba ya watu kwenye mataifa mbalimbali, kwa kuzingatia sheria wamepewa kibali cha kuua pale wanapoona maslahi na usalama wa Taifa vinahatarishwa! Wauaji hawa ni tofauti kabisa na polisi na wanajeshi japo wanaweza kuwa kwenye hayo mavazi. Hawa hawaui kwa uwazi labda mpaka njia zote zinaposhindikana kabisa na muda hautoshi.
Hawa huua kwa siri ama kwa kificho na kutoa taarifa kwenye mamlaka husika, halafu wanaohusika na usalama wa raia hutengeneza story kama ikibidi kufanya hivyo.
Kuna vitengo vitatu vinahusika kwenye usalama na vyote hufanya kazi kwa kutegemeana ama kushirikiana katika baaadhi ya maswala yahusuyo usalama na mengine hufichana kwa sababu maalum.
Kuna usalama wa raia---- POLISI
Kuna usalama wa nchi ----JESHI
kuna usalama wa taifa --- JESHI + POLISI + RAIA
Usalama wa taifa ndio admin wa maswala yote ya ndani na ya nje ya usalama wa nchi. Hawa wako kila mahali na juu ya kila kitu. Lakini utendaji wao ni chini ya zulia ama nyuma ya pazia. Na hawa ndio wana kibali maalum cha kuua kwa maslahi na usalama wa taifa.
Usalama wa taifa kimsingi na kiasili hauchangamani kwa namna yoyote na siasa wala wanasiasa, bali wao wapo kuwachunga na kuwaongoza! Siasa huja na kubadilika lakini usalama wa nchi na taifa hubaki vilevile kwa nyakati zote. Hivyo utendaji na watendaji wake ni vya kaliba ya juu mno, na ndio maana kazi zake si za kutangazwa kwenye vyombo vya habari bali hupatikana kwa mchakato mrefu na mgumu
Kibali cha kuua hakiko kwa watu wa kawaida tu pale inapoonekana kuna kuhatarisha usalama wa nchi kwa kuhujumu nchi, kiusalama, kiuchumi na hata kijamii pia. Kibali hiki kiko hata kwa watu wa kaliba ya juu kama wafanyabiashara wakubwa, wanasiasa mashuhuri, wana sanaa nguli, viongozi mbalimbali wa kijamii na hata wa kidini.
Kimsingi ni kwamba wewe bila kujali nafasi na umuhimu wako kwenye jamii na taifa kwa ujumla, ukianza kuleta zako wanakula kichwa
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye usalama wa taifa na nchi
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye amani ya nchi na taifa
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye umoja na mshikamano wa taifa
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye uchumi wa nchi na taifa
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye nyanja zingine zozote zenye maslahi ya nchi na taifa basi tambua wazi huna maisha marefu.
Usalama wa taifa ndio engine ya nchi, hawa hawako tayari kuona gari linashindwa kusonga kwasababu ya tairi, gearbox, shockup ama kifaa kingine chochote. KIBOVU KITABADILISHWA FASTA!
NB: Just a general discussion. Not aiming anything specific!
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye usalama wa taifa na nchi
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye amani ya nchi na taifa
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye umoja na mshikamano wa taifa
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye uchumi wa nchi na taifa
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye nyanja zingine zozote zenye maslahi ya nchi na taifa basi tambua wazi huna maisha marefu.