Elections 2015 Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

wewe pasco sasa ndio tunaanza kukuelewa,nani anamkubali Lowasa ndani ya ccm zaidi ya wachumia tumbo?,hata baada ya ukweli kudhihihirika kuwa ile ripoti ya kumbeba Lowasa ilikuwa ya kupikwa na Team lowasa,na ina ofisi jengo moja na team lowasa na floor moja na milango inatazamana bado wachumia tumbo mnahangaika kumbeba mtu ambae hata kupanda mwenyewe lift ya lori hawezi.

kama utafiti ule umesema adui namba moja wa nchi hii ni ufisadi na rushwa inakuwaje kinara wa ufisadi awe rais?

mtueleze mnataka kumfanya nini mzee kasori mpaka amekimbia mji wake hapo arusha?:flame::couch2:shame on you
 
Safi sana. Endeleeni kunyukana ivo ivo. Team zote 6 kazeni buti, msikubali.
 

Fahamu kuwa hakuna fisadi yeyote mwenye uthubutu wa kuondoka CCM kwani kufanya hivyo ni kuvuruga maslahi yake. Je Lowasa akiondoka CCM ufisadi wake utalindwa na nani? Nakuhakikishia kuwa mafisadi wote watakufa na CCM yao. Hayo unayosema wewe ni vitisho tu
 
Acheni kila mtu anayetaka urais jina lake lifike pote pale. Safari hii MDAHALO usiwe hiari. Kazi ifanyike usiku na mchana kuhakikisha kila mgombea anapata ulazima wa kushiriki kwa hiari. kwa mfano kupangwe hivi (hapa nachokoza tu ruksa mawazo ya kuboresha):-
1. Midahalo wa siku 3 Sera ya mgombea kuhusu (a) Uchumi wa nchi; kilimo, uzalishaji na biashara (b) Elimu (c) Mambo ya nje.
2. Wagombea wote watashiriki Mdahalo ambao utaratibiwa na neutral body kutoka tanzania au ikibidi kutoka nje,
3. Mshiriki aruhusiwe kuleta muwakilishi au ushiriki utakaosomwa katika maandishi na pointi zake zitazingatia mapungufu haya kutokushiriki mwenyewe
4. Pointi za kushiriki zitapangwa kwamba hata yule atakayeamua kutokushiriki atapata pointi za kushiriki, ya kwanza ni pointi ya kushinda hatua aliyofikia katika kinyang'anyiro cha kutafuta urais.
 
Mpaka sasa bango chafu la Lowassa ni ufisadi, ambalo limeshindwa kuthibitishwa uhalisia wake. Hiyo inawafanya makada na wananchi kuamua kumkumbatia baada ya kugundua mchezo mchafu unaoendelea. Wananchi wanafurahishwa na maamuzi magumu na sahihi aliyo nayo Lowassa kwa Taifa.
 
mbona hutaji wagombea kuelza mikakati dhidi ya ufisadi?


 

Attachments

  • IMG_7349687624889.jpeg
    38.6 KB · Views: 198
Wanataka watuletee jina gani lingine sasa,.? HAIWEZEKANI. EL RAISI.
 
taja maamuzi matatu magumu aliyowahi kuchukua lowasa kitaifa?

na utuambie kwa nini mzee kasori katibu wa nyerere ametishiwa maisha" baada ya kuanika ukweli kuhusu lowasa kukataliwa na nyerere baba wa taifa



 
Alivunja mkataba wa kinyonyaji wa mwaka 1929 na mwaka 1959 wa Misri uliozuia matumizi ya maji ya ziwa victoria na leo hii kanda ya ziwa wanakunywa maji safi na salama; aliamuru ujenzi wa chuo cha UDOM kwa kutumia pesa zetu za ndani na si kutegemea za Billy Gates; uamuzi mgumu wa kuvunja mkataba wa city water na kupelekea uanzishwaji wa kampuni za wazawa za usimamizi wa maji
 
Kazi ni kazi tu mkuu PASCO aijali mlipaji ni nani so long taaluma inatumika, mmoja ya watanzania wakweli kwenye kauli na mtendo ni wewe.

Lowassa amekuwa akijionyesha kukubalika mtaani kwa kushinda ngumi zisizo professional na kweli hizo anaziweza maana kichwa, teke, mahala pakupiga upangiwi we piga tu waanguke. Hila unapopambana ngumi zinazo amuliwa na referee kuna sheria zake za sehemu za kupiga ukifanya foul kuna consequences.

Amuulize David Milliband kilicho muangusha akiwa kama kipenzi cha viongozi wa labour waliokuwa na nafasi za juu na wapiga kura wao bila ya kutumia pesa tena; siasa za vyama zina rules zake na lazima uzieshimu particularly kabla ujavuka mto wa chama vinginevyo ni kutwanga maji kwenye kinu ata ukiletewa form na kila mtu ndani ya jamii kwanza ni kile chama chako je unacheza na rules za ushindi wa ndani kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…