saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,683
- 7,222
Kwenu ni wapi, we ni wa kuachwa tu uendelee na upumbavu na wivu wako. Ktk hivyo vitu ulivyovitaja mji wa Arusha unaulinganisha na mji upi hapa nchini. We poyoyo hufahamu nchi hii. Barabara nyembamba ulikuwa na futi kamba kuzipima? Nataka niwajulishe watanzania ambao hawajafika Arusha, Mjini kati yaani ndani ya CBD ya Arusha hakuna barabara ya vumbi naweza kusema hata moja tofauti na miji mingine hapa nchini. We una kale kaugonjwa kachuki, ila ndg yangu anayejenga miundo mbinu ni serikali na nchi yetu serikali ni moja.Miundombinu mibovu ndani ya jiji la Arusha.
Aibu kubwa pia ni kwamba makusanyo ya mapato ndani ya jiji la Arusha ni makubwa mno lakini fedha hazijulikani zinaenda wap?? Mkurugenzi wa jiji yupo,meya wa jiji yupo,mwenyekiti wa halmashuri yupo!!
- Barabara za lami,ndani ya jiji la Arusha barabara nyingi za lami ni nyembamba na haziendani kabisa na wingi wa magari yaliyopo.
- Barabara za vumbi,jiji la Arusha limezungukwa na barabara za vumbi kila kona,hii ni aibu kubwa sana kwa jiji ambalo ndiyo kitovu cha utalii nchini .
- Stendi za daladala,hapa sio aibu tu bali ni fedhea ya hali ya juu mfano stendi ya hiace ya kilombero,samunge,kisongo,ngaramtoni,mbauda etc stendi zote hizi ni mbovu mno.
- Stendi kuu,hapa ni zaidi ya aibu,stendi hii ni ndogo,chafu etc
- Masoko,hapa pia pana kazi kubwa ya kufanya! Masoko yote yaliopo ndani ya jiji la Arusha yana-miundombinu mibovu kupitiliza.
Wengi mtakubaliana na mimi kwamba ukiondoka Arusha ukarudi hata baada ya miaka mitano utalikuta jiji lipo vilevile hakuna mabadiliko yoyote ya maana!!
Mamlaka husika chukueni hatua tafadhali hili jiji lipo overrated sana,kuna kazi kubwa ya kufanya ili hili jiji liendana na sifa linazopewa.