Licha ya Mapungufu, Sheria Mpya ya Uchaguzi Pia ina Mazuri Yake!, Imerejesha Mamlaka ya Uchaguzi kwa Wananchi, Hakuna Kupita Bila Kupingwa!.

Gari ina misingi yake injini na chases na hii Sheria Ina msingi wake nao ni wasimamizi kutokuwa na mashaka pande zote
 
Pascal sijui kichwa chako kikoje? bado unatafuta wapi wakuone wakupe uteuzi? This is one aspect among a million! How come you praise such a silly single rubbish!
Mkuu The Retired, this is all about being appreciative, kushukuru kwa kidogo ili upatiwe kikubwa!. Kama unanihesabu na mimi ni praise team, nafukuzia teuzi, endelea kuniona hivyo, wenye jicho la tatu who can read in between the lines, wananijua sifukuzii teuzi na Maza mwenyewe niliisha mweleza Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!

Kama mamlaka ya uteuzi ni Rais Samia, mtu mwenye guts kupandisha bandiko kama
HII kweli huyu ni msaka teuzi?!.

Acheni kazi iendelee!
P
 
Hata mm suara la mgombea mmoja Bado Nina mashaka nalo.
Yaan kura zipigwe za ndio au hapana wakati hakuna mawakala wa vyama vingine vya siasa unafikili Kuna uhalali hapo?
Kura ya ndiyo au hapana hairutubishi demokrasi bora chama husika kipewe muda wa kuleta jina jingine ndani ya siku 14 wakishindwa ndipo kura ya ndiyo/hapana ipigwe na mawakala na Tume wahusike kuhesabu kura hizo. matokeo yake yawe na kifungu cha kupingwa mahakamani na mwananchi yeyote
 
Tatizo kubwa la sheria hii ni uchaguzi kendelea kusimamiwa na Wakurugenzi wa majiji na manispaa hapa ni shida kubwa hakuna mabadiliko lakini pia uandikishaji wa wapiga kura kwa vipindi viwili tu, hili zoezi linapaswa lifanywe kuwa endelevu chini ya maofisa wa Tume.
 
Mimi bado sijafurahishwa, kura za ndio na hapana, bado ni kizungumkuti. Watu watapiga ndio tu hata kama hawataki.

Hivi haiwezekani kabisa kama hajatokea mtu kuahirishwa uchaguzi wa sehemu husika mpaka mtu apatikane.
Watu kupiga ndio na hapana kwa mgombea mmoja ni usanii tu kama wa Nyerere na kivuli.

Kwanini kwenye uchaguzi wa vyama vingi wenye demokrasia mtu agombee peke yake ? Eti kisa unakuta mshindani wake kaenguliwa na tume.....hii sio demokrasia.

Hizo hapana zitapuuwa tu, Kuna chama hakitegemei hata kura kushinda.
 
Hapa umenena vyema na hiki ndio kichaka Cha akina Tulia Ackson kujidai kuwa CCM wanamiliki Dola
Swala langu kwa chama changu tawala, hivi tunaogopa nini kuunda tume huru kukawa na uchaguzi huru. Jinsi mtandao wetu ulivyo mkubwa, jinsi wananchi wanavyotuamini tunashindwaje kwenye uchaguzi. Kwa vyovyote vile hawa wapinzani wana kelele tuu. Hawawezi hata kwa miaka 100 kufanikiwa kushika dola. Ushauri wangu ni kuwa tume iwe huru ili tupunguze kelele. Mwisho wa siku tutawauliza kwa mbwembwe sana kuwa, haya tume huru hiyo.na bado mmeshindwa sasa semeni jingine
Wakatabahu
 
Hata kama tumeamua kupaka rangi tu, mbona hakuna tofauti na rangi ya nyuma... Upotevu wa pesa tu.
 
Unafurahia kupewa haki robo au siyo? Wewe ni mwaandishi mnafiki kama unaona jema kwenye sheria zenye mapungufu makubwa yatakayosababisha jamii zetu zikose haki zao za kuchagua viongozi wanaofaa na kutuletea wapuuzi wanaharibu maendeleo yetu na kuingia mikataba mibovu yenye gharama huko mbele siyo tu kwetu bali hadi vizazi vyetu.
 
Mkuu Paskali ni mwanamahakama!! Anavigezo vya kutuelimisha!
NI msomi wa sheria na hajapewa certification ya kutafsiri sheria kama inavyotakiwa.

Tafsiri anayotupa inajikita kwenye tasnia yake aliyosomea na haijikiti kwenye uhalisia na hitaji la wakati.

Sijambeza bali nime-m-challenge
 
NI msomi wa sheria na hajapewa certification ya kutafsiri sheria kama inavyotakiwa.

Tafsiri anayotupa inajikita kwenye tasnia yake aliyosomea na haijikiti kwenye uhalisia na hitaji la wakati.

Sijambeza bali nime-m-challenge
Mkuu Msanii , an advocate is an official of the court, hivyo ni certification tosha kutoa legal opinion, kwa mujibu wa katiba yetu, hakuna certification yoyote ya kutafsiri sheria kwa yeyote zaidi ya Mahakama Kuu!.

Tuna tatizo kubwa sana la legal interpretation, toka kwenye sheria zetu hadi kwa majaji wetu!. Mfano mzuri ni huu- Katiba ndio sheria Mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni batili!.

Mtunga katiba alidhamiria katiba ndio inayobatilisha sheria batili na sio Mahakama Kuu!, kazi ya Mahakama Kuu ni kuthibitisha tuu huo ubatili na kutamka sheria fulani ni batili, tangu baada ya tamko hilo la Mahakama Kuu kuwa sheria fulani ni batili kwa kwenda kinyume cha katiba, anayeibatilisha sheria batili hiyo ni katiba ya JMT na sio Mahakama!. The role of the court is kutamka tuu kuhusu huo ubatili na katiba ndio inaubatilisha!.

Bunge la Tanzania limetunga sheria batili, Mahakama Kuu ikatangaza ubatili huo na kuubatilisha, serikali yetu ikakata rufaa kupinga uamuzi wa huo!, kama katiba ndio sheria Mama, katiba imetamka sheria yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni batili, serikali imetunga muswada wa sheria batili, ikaupeleka huo muswada Bungeni kutungwa sheria, Bunge likatunga sheria batili, Mahakama ikaitangaza ni sheria batili, baada tuu ya Mahakama kutangaza ubatili wa sheria batili, ni katiba ndio inaibatilisha!, hivyo baada tuu ya uamuzi ule wa Mahakama, sheria batili hiyo inakuwa imebatilika there and then!, sasa serikali inapata wapi mamlaka ya kuikatia rufaa katiba?.

Nimejitolea kuendesha elimu ya katiba, sheria na haki ili kuwaelimisha Watanzania waijue katiba yao, sheria zao na haki zao, ili waweze kutimiza wajibu wao!.

Somo la kwanza ni kuijua katiba ni nini, katiba ni ya nani, na mamlaka ya katiba ni yapi na yametoka kwa nani!. Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni nini, ya nani, ya kazi gani? Msemo "Katiba ndio kila kitu" Una maana gani? Katiba ina umuhimu gani?

Somo la pili nikaendesha kuhusu katiba ni sheria Mama, maana yake ni nini?. Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama?

Na baada ya ubatili huo kutangazwa na Mahakama Kuu, serikali yetu ikakata rufaa, ikashindwa!. Ikauchukua ubatili huo na kuuchomekea kiubatili ndani ya katiba yetu!.

Mahakama Kuu ikakata na kutoa uamuzi kuwa sheria hiyo ni batili na uchomekea huo wa batili ndani ya katiba yetu pia ni batili!. Serikali ikakata rufaa ikashindwa tena!.

Kwa vile Jaji Mkuu anateuliwa na rais, serikali ikaomba review ya Mahakama ya rufaa, na Mahakama ya Rufani ikiongozwa na CJ mwenyewe akisaidiwa na majaji 7, Full Bench, wakatoa uamuzi wa ajabu kabisa kuwahi kutokea!, eti Mahakama haina uwezo wa kuliingilia Bunge kwenye jukumu lake la utungaji wa sheria, kama Bunge limetunga sheria batili na kufanikiwa kuipenyeza mpaka kwenye katiba ya JMT, then, Mahakama haina mamlaka ya kuingilia hilo ni Bunge lenyewe ndio lirekebishe!.

Yaani katiba ivunjwe na Bunge kwa kutunga sheria batili kinyume cha katiba, halafu kikauchomekea ubatili huo kiubatili ndani ya katiba yetu!, Mahakama yenye uwezo wa kutamka ubatili huo, inaligwaya Bunge!, sasa ndio serikali inaleta sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ule ule!, unategemea nini?!.

P.
 
Bila kupingwa

Ule utaratibu ulikuwa ni wa kishetani sana

Hata Nyerere hakuwahi Kupita bila kupingwa [emoji23]

2025 tutaona wagombea wa CCM wakipitishwa wao tu kisha siku ya uchaguzi ajapigiwa kura yy tu,sasa hii ina tofauti gani ya kupita bila kupingwa?
Akipigiwa kura yy tu DED atamnyima kutangazwa?
Mnajidanganya sana watz,CCM ingekua na nia njema ingeondoa mchskato mzima wa uchaguzi mikononi mwa DED ambao siku hizi wanateuliwa hadi Wenyeviti wa CCM kiwa DEDs
 
Wenzako wanaangalia Maokoto

Awe na mshindani au Peke yake lazima amwage mpunga 😂
 
Haya ni maoni kikada, carefully crafted. Unataka kutuweka kuwa victims wa ujanja ujanja wa CCM.
 
Uko Right Kwa nchi yenye mfumo wa vya vyingi,swala la mgombea 1 kupita na kubigiwa kura ya Ndio or Hapana ni uhuni tu, si kweli vyama vyote eti Mgombea apite awe mmoja ni dalali za rushwa na njia yakupata ushindi wa mezani.
 
Wananchi wa Bukombe,
Tunaitumia serikali na CCM Salaàm za Mwaka Mpya wa 2024.

Lkn pia tunasema 2025 hapa Bukombe ndani ya CCM na ikiwezekana uchaguzi Mkuu iwapo atakuwa tayari kuendelea kuwa mbunge basi asipaswe kuwa na mpinzani. Kazi alizofanya ni nyingi sana lkn kubwa zaidi amewekeza kwa wananchi (Sisi).

Pamoja na kuwa uchaguzi ni jambo la kikatiba lkn si lzm kumsumbua kiongozi huyu - CCM Bukombe imeungana, madhehebu ya dini yameungana, taasisi za umma zimeungana" mambo yako safiiiii".

Tutasikika!
 
Amefanya nini Bukombe?
 
Mmeanza so ndio!!?
Majaliwa ndio mgombea 2025 Hilo lipo wazi!

Biteko no waziri mkuu!!

TEC wakizingua tunamweka Gwajima,wakileta udini!!

Tuna plan A na Plan B!

Mkileta wenge hasa mkojani akikomalia Bas wale jamaa watachukua tulale saa 12:00 jioni!

Mbingu,mawe na vitu vyote vimekubali haya!!
Tunasubiri kwa uvumilivu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…