Licha ya vikwazo kadhaa, hatimaye nimefanikiwa kuianza ile safari. Asanteni kwa sala zenu zimesaidia ila bado zinahitajika sana! Mungu nisaidie

Licha ya vikwazo kadhaa, hatimaye nimefanikiwa kuianza ile safari. Asanteni kwa sala zenu zimesaidia ila bado zinahitajika sana! Mungu nisaidie

Daima mbele nyuma mwiko
Wanabodi,

Ukiwa na jambo lako, ukaomba msaada wa usaidizi kwa public ili usaidiwe, the public ulioomba msaada ika respond positive, ukasaidiwa kwa michango ya hali na mali, baadhi yetu ni huwa wanyenyekevu wakati wa kuomba tuu, lakini tukisha fanikiwa, tunatabia ya kujisahau. Haturejei kushukuru na wala hatukumbuki fadhila na kuwa na shukrani, naomba mimi nionyeshe tofauti kwa kurejea humu kushukuru.

Mimi nilikuja kwenu humbly kuomba msaada wenu, Wana JF, niko mbele yenu kwa unyenyekevu kuomba baraka zenu & moral support yenu jambo langu hili liwe! Mniombee Mungu asaidie, awezeshe liwe!
na kweli nimesaidiwa, nimefanikiwa na sasa narejea kwenu kwa unyenyekevu tena kushukuru kuhusu lile "jambo langu jambo letu".

Licha ya vikwazo kadhaa vidogo vidogo vya hapa na pale, hatimaye nimefanikiwa kuianza ile safari. Asanteni sana kwa sala zenu na michango yenu. Sala zenu na michango yenu vimewezesha, nimefanikiwa kwa asilimia 100% kutimiza lengo kusudiwa la kuianza safari. Ila sala na moral support bado vinahitajika sana katika muendelezo hadi jambo letu litimie, Mungu nisaidie!

Mwanzo siku zote ndio huwa mgumu, sala zenu na support zimesaidia sana katika hatua hii ya mwanzo ila huko mbele tunakokwenda, kama tumeanza vizuri, then mbele ni msesereko tuu! Tumeanza na Mungu, tunaenenda na Mungu na tutamaliza na Mungu.

Juzi ndio juzi, yaani juzi was the day ya kuanza ile safari ya lile Jambo letu! Japo nimeianza safari kwa vikwazo vidogo vya hapa na pale, lakini nimekamilisha hatua ya kwanza japo kwa mbinde! Tulikotoka ni kurahisi, tunakwenda ni mbali na kugumu zaidi, hivyo nakuomba keep praying for me. Ungana nami morally, to offer me your unconditional support kwa kujitolea will power yako, tuunganishe nguvu, join forces za will powers za wengine wenye mapenzi mema na taifa hili to produce a gigantic power of forces of will, that will make things happen! Mungu nisaidie!

JF ilipoanzishwa, na mkuu Max Ile 2006, was meant to be a home of great minds, lakini kwa vile watu hatulingani kuna simple minds, kuna ordinary minds na kuna great minds. Vivyo hivyo, humu JF tuko watu wa aina zote, simple minds wanao discuss people, ordinary minds wanao discuss events na great minds hawa wana discuss ideas, wote tuko humu na tumekuwa accommodated.

Bado silitaji hili jambo langu, na all ma GT wameisha lielewa na hawalisemi. Wale wenzangu na mimi ma ordinary minds wao watalizungumzia as an event! Nawaomba hata kama wewe ni mmoja wa ordinary minds, kama unajihisi unalijua, hilo jambo langu, nakuomba jifanye GT kwa kutolisema! Na wale simple minds ambao kazi yao is to discuss people, I beg you, don't discuss people, hapa usimjadili mtoa mada, muombee tuu afanikiwe katika jambo letu.

Japo siamini katika uwepo wa nguvu za giza ila kiukweli nguvu za giza zipo, they exist in reality and to those who believes them, they can act on you and destroy your dreams! Even if you don't believe them, kwa vile hizi nguvu zipo, they can act on you, zikakukumba na kukutandika, na kukukwamisha kwa kukuchelewesha tuu lakini haziwezi kuzuia! Kama jambo letu limepangwa na yeye, then ni limepangwa na litatimia!

Kwa vile mimi ni mtu wa ma story, kama wewe sio mtu wa mastory mastory then ishia hapa! Kama wewe ni mtu wa mastory, endelea...

Sikiliza, hiki ni kisa cha kweli kilichotokea juzi na jana kuhusiana na jambo letu hili!​
Kitendo cha kusafiri huku nimetinga sare za chama mwanzo kulinipa taabu, maana zamani kuvaa sare za chama ilikuwa aibu hivyo nikawa naona soo. Kumbe kusafiri na sare za chama sasa ni opposite, badala ya aibu ni advantage. Kwanza kufika airport nikapokelewa kama Mheshimiwa, walidhani mimi ni Mheshimiwa Mbunge, hivyo ule ukaguzi wa vua mkanda, vua viatu huo uliniepuka.

Kufika boarding area nikapelekwa Tanzanite lounge, na baada ya ku-board yule flight attendant hakubodha kuangalia boarding pass yangu, tiketi yangu ni economy, ila kufuatia sare niliovaa nikawa upgraded to Business Class, makamuzi yakaanzia kwenye ndege!

Kufika Songwe napokelewa na kupelekwa VIP, kule nikakutana na Mawaziri, RC na wakubwa, hivyo nami kuonekana kama mkubwa fulani huku nikiitwa Mheshimiwa. Hivyo ndugu zangu, pamoja na ule mwanzo mgumu wa safari hii, hizi sasa ni dalili nzuri za kufunguka kwa njia, sasa mwendo ni msesereko tuu wa praaaaa mpaka Maka!​

Paskali - 0754 270403
 
Nakutakia kila la heri ukipita ntakuwa nakuja Nairobi, sky lounge au Dolce kule Koinange tunapata moja baridi ....
 
Paskali nakuheshimu ila hapa nyuma njaa iliharibu image uliyojitengenezea, itakuwa ni kazi kukikimbia kivuli chako mwenyewe
 
Back
Top Bottom