Hivi ni nani huyu aliyesema mwanamke hana haki kwa mali ya mume wake ambae alishirikiana nae kuzalisha mali!!
Hii kauli ya "mali ni kwa ajili ya watoto" ni kauli ya kuwaridhisha walafi wa mali za marehemu hususani wale wanaotoka upande wa mwanaume!!!
Hawa walafi ni kawaida wakishaona ndugu yao umekutwa na umauti, wao ndo watataka wapewe wakati hawana haki hiyo, at least from western culture iliyokuwa adapted na mahakama zetu za ki-secular.
Ili kuwaridhisha, inaonekana bora kuwaambia hizi mali ni kwa ajili ya watoto labda wanaweza kuingiwa na moyo wa imani kwa kuona hao ni watoto wa ndugu yao!!!!
Lakini kimsingi, kama mwanamke ameshiriki kwenye kuzalisha mali lazima na yeye awe na fungu lake hapo let alone fungu la watoto!!!
Na kama ni sheria za kiislamu wala haijalishi kama huyo mwanamke alizaa na marehemu ingawaje mwanamke aliyezaa na marehemu anapata fungu kubwa ukilinganisha na yule ambae hakuzaa nae! Na wala hawaangalii kama alizalisha nae (mali)! Haya mambo ya kuzalisha nae mali yanaangaliwa kwenye talaka na sio urithi!!!
So, kama Zari alifunga ndoa na Ivan na walichuma mali pamoja lakini wakati wanatengana hawakugawana mali; basi hapo Zari ana chake as a business partner let alone fungu la watoto!!!!
Huyo King Lawrence ni kiwakilishi tu cha Waafrika waroho wa mali za marehemu na ndio maana jana nilisema hapa Zari na wanawe watakuwa wameshanyamaza kulia lakini King Lawrence anaendelea tu!!!!