Linapokuja suala la ujasiliamali ni mazao yenye majina makubwa tu kama matikiti, vitunguu na Tomato hutajwa! Nyanya chungu ni zao lisilovuma sana japo linawatoa sana wakulima na linawalaji wengi sana. Nyanya chungu mfano aina maarufu kama YEBOYEBO ni zao linalonivutia sana kwa sifa zifuatazo:
1. Afrika ni nyumbani kwao linazaa sana hata wakati wa joto kali ambapo kwa tomato na hoho hubabuka sana kwa jua
2. Tomato na Hoho hupunguza sana kutoa maua na matunda kwenye joto kali YEBO YEBO hupeta tu
3. Mazao mengi ya bustani huhitaji madawa ya ukungu kupita kiasi majira ya mvua, nyanya chungu hazideki ki hivyo
4.Tomato na hoho usafirishaji wake ni kama mayai, nyanya chungu zisafirishwapo mara nyingi watu hukaa juu yake
5. Kipindi cha kuanza kuchuma hadi mmea kuchakaa kwa aina nyingi za tomato ni mwezi mmoja, hoho zenye ubora ni miezi 2, lakini nyanya chungu huchumwa kwa zaidi ya miezi 8 ili mradi zinamwagiliwa maji na mbolea.
6. Wakati bei ya Tomato ikianguka mkulima nae hugalagala chini asisimame tena lakini nyanya chungu haimtupi mkulima kivile
Kwa wenye mitaji midogo wanaotaka kuikuza ili waweze kupata nguvu kubwa ya kilimo bila kuwa na presha inayopanda na kushuka Nyanya chungu ni zao lenye uhakika mkubwa!
Swali ni kwa nini zao hili halitajwi sana yaani halivumi ?