salimkabora
JF-Expert Member
- Nov 10, 2012
- 2,441
- 652
Ufufuo ni habari mpya alizokuja nazo Yesu na baadaye kuthibitishwa na Muhammad s.a.w ila maisha baada ya kifo hayajafafanuliwa sana na kilichowazi ni kwamba kifo ni usingizi hadi ufufuo. Baada ya huo wale wabaya wataharibiwa kwa moto na sayari yao kukunjwakunjwa kama karatasi na kutupiliwa mbali. Wema watabakia, na mbingu mpya na nchi mpya vitashuka toka mawinguni na makao ya mungu yatakuwa pamoja na wanadamu. Lipi ni lipi kati ya watu wema kupaishwa hadi mbinguni kuishi na mungu au mungu kushusha makao kuishi na wanadamu sioni kama ni muhimu ili mradi zawadi ya mwisho ni ileile ya wema kuwa na makao ya milele na mungu. Kutakuwepo na kipindi watu wataoa na kuzaa watoto lakini kipindi hicho nacho kitakuja kukoma pale makusudi ya awali ya mungu yatakapokuwa yametimizwa. Raha zitakuwa nyingi lukuki na wala kukoma uzazi haitakuwa ni kasoro na wala sidhani itakuwa ndio ukomo pia wa watu kujamiiana. Hapo nimetia akili yangu mwenyewe kidogo baada ya kulitafakari vizuri lile kusudi lililo kuu la mungu. Kusema ufufuo ni habari mpya sio mawazo yangu chunguza agano lote la kale uone kama kuna nabii aliyekuwa anaongea habari za siku ya hukumu au kiama si Daud, Musa, Yoshu, Ibrahimm, nk. ambae alitaraji kwenda moja kwa moja mikononi mwa mungu au ndani ya himaya yake. Wote waliamini mwisho wa yote ni kaburi.