Movic Evara
Senior Member
- Jan 31, 2018
- 197
- 431
Mshua hana utani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
thank you mtani
Ok, ntaandika nikipata muda humu humu,,, ntaandika jinsi nilivyokutana na mjeshi mmoja jambazi aliyewahi kusumbua sana miaka ya nyuma anaitwa kamanda dogo na story yake humo ndani..... Ntaelezea upande ambao haujawahi kuelezwa na hisia zake juu ya mauaji aliyowahi kufanya na mahusiano yake ya mapenzi.Andika tu 😊
Andika tu 😊
Mkuu sinaga longolongo nao na nawaeleza uhakika. Namaaanisha nachokisema na wako kama wawili walishakutana navtimbwili langu vemaMkuu kama unataka yaishe uendelee na mishe zako ww wape tu hao jamaa Huwa wanasema wanazaidi ya makosa 1000 ambayo Yako wazi kukubambikia kwahiyo wee wape tu usepe zako hawashindwi kukubambikiza kosa ambalo hujafanya likakupotezea muda wako,, niwashenzi sana hao jamaa. Si Kila aliyeko mahabusu ama jera kwamba ametenda kosa wengi wamo humo kwa makosha ya kubumbiwa
This is a master piece to write...andika tunasubiri Kwa hamuOk, ntaandika nikipata muda humu humu,,, ntaandika jinsi nilivyokutana na mjeshi mmoja jambazi aliyewahi kusumbua sana miaka ya nyuma anaitwa kamanda dogo na story yake humo ndani..... Ntaelezea upande ambao haujawahi kuelezwa na hisia zake juu ya mauaji aliyowahi kufanya na mahusiano yake ya mapenzi.
.Portion 21:
.....Kipindi bado nafatilia likizo yangu, nikaamua kwenda kumtembelea Mr. B maana nae tulikuwa na muda kiasi hatujaonana. Kama ambavyo imekuwa siku zote ninapoendaga kwake, huwa ananiongezea vitu kichwani. Iwe ni kwa maongezi au ushauri.
Kwavile nilitaka niongee nae kwa muda mrefu, hivyo nilienda mapema nyumbani kwake.
Mr. B: "Karibu sana Amphibian"
Mimi: "Asante sana, nimekuja kukuaga Mzee"
Mr. B: "Kuniaga? Unaenda wapi?"
Mimi: "Siku sio nyingi nitaanza likizo, hivyo nitakuwa nje ya mkoa kwa mwezi mzima"
Mr. B: "Ooh ni jambo zuri sana. Kwahiyo unaenda wapi?"
Mimi: "Naenda kijijini kuwaona wazee"
Mr. B: "Hivi wazazi wako wote wapo?"
Mimi: "Ndio"
Mr. B: "Ni jambo la kheri kutumia muda wako na wazazi wako. Naamini kuna mengi utachukua kwao"
Tukaendelea kupiga story zingine za maswala ya biashara, kijamii nk. Pia tulipata nafasi ya kwenda shambani kwake ambako analima na kufuga. Mida ya jioni wakati tukiwa ndani ya gari tunatoka kule shambani akaniuliza:
Mr. B: "Biashara inaendaje sasa hivi?"
Mimi: "Tunajikongoja taratibu, japo mambo ni magumu"
Akaniangalia kwa muda bila kusema chochote. Ikabidi nimuulize vipi?
Mr. B: "Mna muda gani tokea mmesitisha huduma kwenye kampuni yenu?"
Nikashangaa amejuaje kama tumefunga biashara? Maana ni kweli tulikuwa na takribani miezi mitatu au minne tokea tumesimamisha huduma.
Mr. B: "Kuna kazi nilitaka ifanywe na kampuni yenu, ila nikaambiwa imesimamisha huduma kwasasa. Shida nini?
Mimi: "Gharama za uendeshaji zilikuwa juu, tukaamua kusimama kwa muda. Ila tutarudi tena".
Mr. B: "Fanyeni haraka irudi tena, vinginevyo itakufa moja kwa moja"
Mimi: "Sawa Mzee"
Baada ya ukimya mfupi, akaniuliza swali jingine:
Mr. B: "Hivi ni kitu gani ambacho unakihofia sana kwa upande wako?"
Sikutegemea ilo swali, hivyo nikajikuta nimekaa kimya kidogo. Kisha nikamjibu "Labda kifo"
Mr. B: "Labda? Kwamba huna uhakika?"
Mimi: "Sijawahi kufikiria juu ya vitu ninavyoogopa"
Mr. B: "Na kwanini uogope kifo? Maana siku uliyozaliwa ilijulikana kwamba kuna siku utakufa"
Kabla sijaongea chochote, akaendelea:
"Ushawahi kujiuliza itakuwaje ikitokea siku huwezi kabisa kwenda kazini?"
Mimi: "Nitatafuta njia nyingine ya kutengeneza hela"
Mr. B: "What if afya hairuhusu kuendelea kufanya kazi?"
Mimi: "Aisee, hapo kidogo itakuwa mtihani"
Mr. B: "Ushawahi kufikiria utaishije baada ya kustaafu?"
Mimi: "Hapana, ila mpaka muda huo ukifika nitakuwa nimeshajipanga"
Mr. B: "Kipi kina kuzuia kujipanga sasa hivi?"
Mimi: "Mbona mapema sana Mzee? Yani nianze kufikiria kustaafu leo hii?"
(Akacheka kidogo)
Mr. B: "Kuzaliwa kwako yawezekana wazazi wako hawakuwa wameplan, hivyo ujio wako ulileta presha na malumbano kwao. Umesoma shule under presha, pengine kozi uliyosoma siyo uliyokuwa ukiitaka, umetafuta kazi kwa presha, unafanya kazi kwa presha, bado pengine utaoa kwa presha. Tena leo hii bado unataka uje kustaafu kwa presha ingawa tayari unajua ni lini utastaafu. Ni lini utajifunza kupangilia mambo yako?"
Sikuwa na jibu, nikajikuta nimetulia kimya. Kwa dakika kadhaa nikajikuta nafanya review ya maisha yangu. Ni lini nilifanya mipango yangu kwa utulivu? Mara zote nimekuwa kama gari inayowashiwa kwenye gia. Nimekuwa high high muda wote tu.
Na kiukweli nikifikiria alichosema, sikuona kama kuna ubaya kuanza kujipanga na kustaafu japo bado kuna miaka mingi mbele.
Mr. B: "Mbona umekuwa kimya ghafla?"
Mimi: "Sijawahi kuwa na fikra hizo, hivyo wazo lako limeclick kwenye akili yangu"
Mr. B: "Bado hujachelewa, anza kulifanyia kazi kipindi ukiwa bado una nguvu"
Mimi: "Tatizo sijui nianzie wapi. Kama hautojali naomba unishike mkono kwenye ili pia. Nahitaji muongozo wako, naamini kuna namna unaweza kunisaidia"
Mr. B: "Usijali, nenda likizo yako. Ukirudi tuna vingi vya kuweka sawa.
Akanidrop CBE, kisha akaendelea na safari yake kuitafuta Kisasa. Nikaita boda anisogeze maghettoni kwangu. Ila muda wote kichwani nawaza kumbe kuna vitu vingi vya kufanya ambavyo sijawahi kuvifikiria? Nikajikuta nina deni kwangu.
"Kuna siku itafika nitahitajika kustaafu. Ila nitastaafu vipi?"
Nikagundua ninavitu vingi sana nahitajika kuvifanyia kazi kwenye maisha yangu. Nahitaji kujipanga sasa kwa ajili ya baadae.
Najipangaje?! Ili swali lilinipa nguvu mpya. Kwavile Mr. B ameahidi kunishika mkono, huyu anazidi kuwa mtu muhimu sana kwangu. Acha nizidi kuwa nae karibu.
***** ***** ** *** *****
Siku mbili tokea nimetoka kuonana na Mr. B, Katrina alinipigia simu mida ya usiku. Ilikuwa around saa nne au tano kasoro, maana nilikuwa nishaanza kusinzia kabisa.
Mimi: "Hallo, niaje?"
Katrina: "Fresh tu, nimepiga muda mbaya?"
Mimi: "Nilishasinzia tayari, ila sio mbaya niambie"
Katrina: "Nina mimba"
Usingizi ulikata pale pale. Nikabaki kimya kwa muda, maana sikujua niseme nini.
Katrina : "Vipi mbona kimya?"
Mimi: "Amna nimekuwa surprised tu. Vipi ina muda gani?"
Katrina: "Sio muhimu ilo. Nilitaka tu kukupa taarifa, wewe lala tutaongea vizuri Kesho"
Mimi: "Sasa kama ungetaka tuongee Kesho why umepiga leo? Hebu niambie inamuda gani sasa?"
Katrina: "Nilipiga kwasababu sipo sawa, na nilihitaji mtu wa kuongea nae"
Mimi: "Uko wapi sasa hivi?"
Katrina : "Nyumbani"
Mimi: "Umeshawaambia home?"
Katrina: "Hapana. Kesho nitakuja tuongee vizuri. Sasa hivi endelea kulala"
Maongezi yetu yaliishia hapo, akakata simu. Ila usingizi ukawa umeyeyuka, nikajawa na mawazo.
Hii mimba mbona kama itaniharibia mipango yangu? Kivyovyote vile, hii inaweza ikawa ni sababu kubwa ya kumfanya Mr. B aniozeshe binti yake, ila sisi hatukuwa tayari kuwa pamoja. Isitoshe Katrina yupo kwenye mahusiano.
Sio kwamba nilikuwa naogopa au nashindwa kulea ile mimba, ila kilichonipa wasi wasi ni matokeo yatakayoambatana na hii mimba.
Asubuhi kama kawaida nikaenda kazini, ila muda wote nilikuwa naangalia simu maana nilitegemea kutafutwa na Katrina. Ila mpaka inafika mida ya mchana hakunitafuta, nikaamua kumpigia hakupokea. Nikamtumia ujumbe kwamba akiwa free anipigie. Ujumbe ulifika, ila mpaka siku inaisha hakunitafuta.
Nikajisema chochote kitakachofatia sawa tu, acha niendelee na mambo yangu.
Ikapita kama wiki hivi, hapo ikawa muda wowote naweza kusafiri. Hiyo siku nilikuwa natoka kwa jamaa yangu, nikaona nipitie kwa Mr. B ili nimpe Hi, japo lengo kubwa ilikuwa ni kumuona Katrina.
Nilienda siku mbaya.
Maana nilikuta Mr. B amefura jicho jekundu, amekaa kwenye bustani yake mezani kuna bapa la konyagi kubwa. Kabla hata hatujasalimiana vizuri:
Mr. B: "Watoto wa siku hizi ni disappointment tupu"
Mimi: "Kwanini unasema hivyo Mzee?"
Hakunijibu, akawa ametulia.
Mr. B: "Huyo mwenzako huko ndani amefanya mambo ya kipuuzi sana, kiasi kwamba hata kumuona sitaki"
Akili ikaanza kuniambia tayari mimba ishajulikana. Ila kwanini amevimba hivi wakati binti yake ni mtu mzima sasa?. Nikashindwa niongee nini. Ila wakati nipo kimya, akaendelea:
"Hivi mtu mwenye akili zake timamu anawezaje kutoa mimba?".
Ile kauli ikanishtua. Katrina ametoa mimba? Kwanini sasa? Mbona hata hakunishirikisha tukaongea?
Mimi: "Ametoa mimba?"
Mr. B: "Yani nimekuwa disappointed kuliko ninavyoweza kusema. Sitaki hata kumuona mbele yangu"
Nikajikuta najiuliza, why Katrina amefanya vile? Japo nilikuwa kama najiuliza mwenyewe, ila Mr. B alisikia nilichosema:
Mr. B: "Nenda kamuulize mwenyewe, yupo ndani huko"
Mimi: "Muache tu kwasasa, sina mazoea nae, sidhani kama italeta maana kuongea nae"
Ile kauli ilimkwaza sana Mr. B:
Mr. B: "Hebu acha kuongea upuuzi na wewe, rudi ulipotoka, sasa hapa umekuja kufanya nini?. Yani mwanaume unashindwa kuongea na mtoto wa kike kisa hujamzoea?. Mmekuwa dhaifu sana, no wonder why utoaji mimba umeongezeka. Mwanamke hawezi kutoa mimba kama mwanaume unasimama kwenye nafasi yako"
Nikataka nimjibu ila kwa hali aliyokuwa nayo nikahisi hapa nitaendelea kumtibua. Ikabidi nimuulize Katrina yuko sehemu gani. Akanijibu kwa ishara akinyooshea kidole ndani, alafu akanyanyua bapa lake na kulinywa dry. Ikabidi niingie ndani.Nikamkuta Katrina yupo chumbani kwake. Nikaingia, namkuta kasimama karibia na dirisha. Ni kama alikuwa anatusikiliza wakati naongea na Mzee wake.
Mimi: "Mambo vipi?"
Katrina: "Safi tu, karibu"
Mimi: "Asante, umekuwa ukija kwangu mara nyingi, hatimae leo nimekuja kwako"
Akatabasamu tu bila kuongea chochote.
Mimi: "Mbona ulikuwa hupokei simu zangu? Na imekuwaje umefikia uamuzi huu?"
Katrina: "Nilikuwa stressed, so nilihitaji utulivu"
Mimi: "Na baada ya kutulia ndio ukaamua utoe mimba? Why?"
Katrina: "Sikuwa na namna"
Mimi: " Kivipi? Kwanini usingenishirikisha?"
Katrina: "Sikuwa na uhakika mimba ilikuwa ya nani, yako au ya my bf"
Nikabaki kimya kwa muda.
Katrina: "Kwako nilikuwa nakuja, na kwake pia nilikuwa naenda"
Mimi: "Hata hivyo hukutakiwa kufikia uamuzi huu. Angalia sasa situation uliyojiweka"
Katrina: "Hii itapita tu. Ni heri nivumilie lawama za sasa kuliko fedhea za mbeleni. Unadhani mtoto azaliwe alafu awe wa kwako na sio wakwake, hiyo aibu ingeambatana na Mimi kwa maisha yangu yote"
Nikabaki tena kimya kwa muda.
Mimi: "Ila Mzee amemind sana"
Katrina: "Atapoa tu, hakuna namna"
Mimi: "Ilikuwaje wakajua kama umetoa?"
Katrina: "Kuna mistake nilifanya"
Mimi: "Mistake gani?"
Katrina: "Niliangusha kile kipimo, alafu mama akakiokota. Akahisi ni cha dada wa kazi, ila alivyomuuliza akakataa. Mama hakumuamini, akampima tena. Kipimo kikaonesha dada hana mimba. Humu ndani wanawake tupo watatu tu, hivyo kama sio mdada wa kazi, moja kwa moja jibu likawa ni Mimi"
Nikabaki kimya tu namsikiliza:
"Hawakunipigia simu kuniuliza maana sikuwa nyumbani muda huo. Na niliporudi, Mama alikuwa ametoka. Sikuwa najua chochote, mida ya saa tatu usiku nikatumia vidonge kisha nikajilaza. Mama aliporudi, akaja direct mpaka chumbani kwangu kuniuliza habari za mimba. Akanikuta maumivu ndio yamekolea, nikajaribu kumuongopea kwamba nipo period. Wakati tunaendelea kuongea, akaona kasha la dawa nilizomeza. Hapo ndio msala ulipoanzia".
Mimi: "Aisee, vipi na Jamaa yako ulimwambia kama una mimba?"
Katrina: "Hapana."
Mimi: "Mzee wako ameniambia nije kuongea na wewe huku ndani, sasa sijui nitampa jibu gani nikitoka"
Katrina: "Mwambie sijaweza kuongea chochote"
Mimi: "Okay sawa acha niende, tutawasiliana"
Katrina: "Okay poa"
Nikatoka mle chumbani, nafika nje Mr. B hakuwepo. Nikaulizia, naambiwa ametoka na gari. Sikutaka kumpigia, nikaamua kuondoka.
Situation ya Katrina ilinipa wakati mgumu sana, sikutarajia kama angefanya vile. Pia nikabaki najiuliza, itakuwaje endapo Mr. B kwa namna moja au nyingine akifahamu kwamba Mimi pia nimechochea ili jambo? Hapo si ndio itakuwa mwisho wa kila kitu?. Sikutaka hata kuendelea kuwaza sana, nikasubiria hatma ya kitakachotokea.......
Naona umetumis sana Aposto...tumeitikia wito maana sio kwa kutuita huku😃😀😀😀
Tangu ulivyoanza kuelezea kufanya mazoezi na Katrina sijui mnaenda chimwaga ndogo nikajua Moja Kwa Moja ulikuwa unafanya kazi Dodoma, inawezekana ulikuwa unaishi mtaa wa makulu na mlikuwa mnakimbia kupandisha mlima wa udom.🫣🫣Portion 21:

Daaahhh Fupi lkn tamu,tupe kipande kinginePortion 21: