Ligi hii imeshaharibika na hakuna Mdhamini kutoka ndani ataekubalika kwasababu ya "Usimba" na "Uyanga"

Ligi hii imeshaharibika na hakuna Mdhamini kutoka ndani ataekubalika kwasababu ya "Usimba" na "Uyanga"

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Ligi kuu yetu imetawaliwa au niseme inaathiriwa na usimba na uyanga, na baada ya GSM kujitoa, mdhamini yoyote ataefuata hataaminiwa na atatuhusishwa na Simba na mgogoro utaanzia hapo (kukomoana).

Si ajabu mwaka huu tukawa na ligi ya hovyo kabisa huku usimba na uyanga ndio ukiwa chanzo.

Kuna timu moja naiona iko tayari kufanya hujuma yoyote kisa tu inaona ina muelekeo mbaya katika ligi na bahati mbaya club hiyo imeshajiona kombe la ligi ni kama lao.

Sasa kitachofuata ni kuonyeshana ubabe baina ya hizi timu mbili na matokeo yake ni ligi kuvurugika.

Bahati mbaya vitabu vidogo ndio vitaathirika zaidi huku hawa mafahari wawili wakiendelea kupeta.

Sometimes natamani hii ligi isimamiwe na wageni wasiokuwa na usimba na uyanga kuondoa huu upuuzi.

Msishangae ligi hii ikashuka/ ikaporomoka katika ubora.
 
Mbona hajakataliwa NBC mkuu? kwani GSM wana lipi la ajabu kuasi cha kusema kuondoka kwao ligi itayumba?

Watu wenyewe hawajatoa hata senti kwenye udhamini wao hewa na wamenufaika kutangazwa na vilabu dhaifu wasio na nguvu ya kuipinga TFF.

Kama si simba kusimama imara hawa jamaa wangevipiga vilabu vyote na huu mkatana wao wa kimangungo
 
Kumbe salary slip una IQ ndogo hiv? Maskini weee mi sikujua!! Kama ulivosema usimba na uyanga hutia upofu kweli wewe ushakuwa kipofu!! Hivi unajua gsm hajatoa chochote katika udhamini huu na timu zinamdai!

Lakini pia timu ziliendelea na ligi bila kuyumba. hivi unajua udhamini wa gsm kila timu ilitakiwa iwe na mgao wa mil3.5 kwa mwezi? Je huo mgao ungesaidia nini kwa club zote za ligi kuu?

Acheni kushabikia mikataba ya kihuni kwenye soka.. tunataka udhamini wa maana ili tusonge mbele bro...
 
Itashuka na kuporomoka kwa namna gani? Yaani mnataka kuaminisha wadau kuwa amesaidia vilabu wakati kwa mujibu wa M/kiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Steven Mguto amesema tangu kuasisiwa mkataba bado hajalipa chochote.

Kumbe wewe Salary Slip unataka kutulazimisha tunaamini Kauli ya Haji kuwa hata uwe na PhD lakini ukiwa Yanga hamnazo..!
 
GSM angeharibu hii ligi kutokana na aina ya udhamini wake

Injinia Hersi anasema piga ua Yanga mwaka huu lazima awe bingwa, afu wakati huo huo mabosi zake GSM wanadhamini Yanga na Vilabu vingne,,, fairness ipo wapi!???
 
Si ajabu mwaka huu tukawa na ligi ya hovyo kabisa huku usimba na uyanga ndio ukiwa chanzo.

Kuna timu moja naiona iko tayari kufanya hujuma yoyote kisa tu inaona ina muelekeo mbaya katika ligi na bahati mbaya club hiyo imeshajiona kombe la ligi ni kama lao.
Mkuu, naona lengo la uzi wako huu, ni KUIZODOA SIMBA!

Mi naona chanzo cha upuuzi wote huu, ni Yanga, na TFF. Hebu tujikumbushe, Yanga walishaikataa nembo ya mdhamini VODACOM, ambao hawana uhusiano na Simba, kisa ina alama ndogo tu, yenye rangi Nyekundu, ambayo ni rangi rasmi ya Simba.

Wakaruhusiwa kuvaa sare zenye nembo yenye rangi waliyoichagua wao! Juzi hapa, wameikataa rangi iliyopo kwenye twiga aliyopo kwenye nembo ya mdhamini NBC. Nayo, kwao imebailishwa rangi, na imekuwa waliyoichagua!

Tujiulize, MO naye aje na udhamini wake, Yanga watakubali kuvaa jezi yenye nembo iliyoandikwa "MO29"?

Sasa, TFF wangesimamia hayo bila kuyumbishwa toka siku nyingi, hivyo viburi vya timu hizi visingekuwepo!
 
Ligi kuu yetu imetawaliwa au niseme inaathiriwa na usimba na uyanga, na baada ya GSM kujitoa, mdhamini yoyote ataefuata hataaminiwa na atatuhusishwa na Simba na mgogoro utaanzia hapo(kukomoana)...
Simba na Yanga zimekuwa kama imani. Kila mtu eight ni simba au yanga.
 
Yanga mmezoea kuburuzwa..Simba walishastukia mchezo na ndio maana wakapinga ule mkataba kwa nguvu zote..hawa GSM wana makandokando mengi sana.
 
GSM kwa akili ya kawaida tu hakutakiwa kuwa mdhamini mwenza wa ligi, na ndio maana huo mkataba wao na TFF wakaufanya siri, sijawahi kuona panakuwepo na siri ya mkataba hata unaowahusu wadau.

Yani mkataba kati ya GSM na TFF kwa vilabu halafu vilabu husika vinafichwa kujua nini kiko ndani ya huo mkataba! huu haukuwa mkataba, ulikuwa ni uhuni na utapeli wa GSM na TFF, shukrani za dhati ziende kwa Simba SC kwa kukataa huu upuuzi.

Mengine uliyoandika kwamba kuna timu yenye muelekeo mbaya kwenye ligi inataka sijui kufanya nini ni hisia zako tu, hazina uthibitisho wowote, wacheni kutetemeka chezeni mpira.
 
Miezi mitatu ya udhamini mwenza GSM hajatoa hata kumi kwa hivyo vilabu, lakini bado watu wanataka kutuaminisha GSM angepunguza njaa kwenye hivi vilabi
 
Tusitishane,Ligi hii ilishawahi kuendeshwa bila mdhamini na ikaenda salama ikaisha,sembuse huyu mdhamini mwenza,suala hapa ni huo mkataba wa ujanja janja, mambo yangewekwa wazi na yangerekebishwa isingekuwa hivi, tulijibiwa kwa kiburi kuwa Mkataba ni wa siri,Wanajuana wao na TFF. Sasa wameshindwana wapj, hatujui
 
Back
Top Bottom