Ligi hii imeshaharibika na hakuna Mdhamini kutoka ndani ataekubalika kwasababu ya "Usimba" na "Uyanga"

Ligi hii imeshaharibika na hakuna Mdhamini kutoka ndani ataekubalika kwasababu ya "Usimba" na "Uyanga"

GSM kajipeleka pale TFF??. Hii ndo tabu ya kutumia utumbo mpana kufikiri
Hatutaki chupli chupli za GSM sheria za udhamini inajulikana ,wakalishe masaburi kigamboni na Yanga yao siyo kuleta chupli chupli kwenye udhamini wa ligi kuu
 
Wewe ugajua reasons za GSM kutolipa hizo fedha? Afu unapuuza 3.5m? Labda umezoea kuhongwa hela nyingi. Zero kabisa
Kumbe salary slip una IQ ndogo hiv? Maskini weee mi sikujua!! Kama ulivosema usimba na uyanga hutia upofu kweli wewe ushakuwa kipofu!! Hivi unajua gsm hajatoa chochote katika udhamini huu na timu zinamdai!

Lakini pia timu ziliendelea na ligi bila kuyumba. hivi unajua udhamini wa gsm kila timu ilitakiwa iwe na mgao wa mil3.5 kwa mwezi? Je huo mgao ungesaidia nini kwa club zote za ligi kuu?

Acheni kushabikia mikataba ya kihuni kwenye soka.. tunataka udhamini wa maana ili tusonge mbele bro...
 
ugajua reasons za GSM kutolipa hizo fedha? Afu unapuuza 3.5m? Labda umezoea kuhongwa hela nyingi. Zero kabisa
Haya sawa mwerevu kutoka utoh. nimekupa na like za kutosha
 
Ligi kuu yetu imetawaliwa au niseme inaathiriwa na usimba na uyanga, na baada ya GSM kujitoa, mdhamini yoyote ataefuata hataaminiwa na atatuhusishwa na Simba na mgogoro utaanzia hapo (kukomoana).

Si ajabu mwaka huu tukawa na ligi ya hovyo kabisa huku usimba na uyanga ndio ukiwa chanzo.

Kuna timu moja naiona iko tayari kufanya hujuma yoyote kisa tu inaona ina muelekeo mbaya katika ligi na bahati mbaya club hiyo imeshajiona kombe la ligi ni kama lao.

Sasa kitachofuata ni kuonyeshana ubabe baina ya hizi timu mbili na matokeo yake ni ligi kuvurugika.

Bahati mbaya vitabu vidogo ndio vitaathirika zaidi huku hawa mafahari wawili wakiendelea kupeta.

Sometimes natamani hii ligi isimamiwe na wageni wasiokuwa na usimba na uyanga kuondoa huu upuuzi.

Msishangae ligi hii ikashuka/ ikaporomoka katika ubora.
[https://res]

MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi Kuu Bara, Steven Mnguto, ameibuka na kusema licha ya wadhamini wenza Kampuni ya GSM kutangaza kujiondoa katika udhamini lakini hakuna klabu yoyote iliyolipwa.


Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tangu GSM watangaze kujiondoa kudhamini klabu za ligi ambazo awali waliingia mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh 2.1Bil.


Akizungumza na Championi Jumatano, Mnguto alisema kuwa, hilo suala wamepanga kulizungumza hivi karibuni
mara baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) watakapokutana.


Mnguto alisema kuwa, wanasubiria wanasheria wao walipitie suala hilo na mwisho wa siku watalitolea ufafanuzi
kwa undani.


“Kiukweli tangu tuliposaini mkataba na GSM nikiri klabu hazijapata chochote. Klabu zimeitangaza GSM kwa muda wa miezi mitatu sasa, kwa hiyo tunasubiri wanasheria walipitie suala hilo tujue tunafanyaje.

“Hata suala la zile nembo kwenye mabega sijui kama zinaweza kutolewa haraka lakini hata hilo litafanyiwa
kazi kisheria,” alisema Mnguto.

Naye Mkurugenzi wa Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura, akizungumzia hilo alisema: “Sisi
baada ya kupata barua kutoka GSM, suala la mkataba ni Bodi ya Ligi na ni vema akatafutwa Mnguto lakini
kwa upande wa sisi TFF hatuwezi kuzungumzia kila jambo.


“Tayari tumetoa tamko letu jana (juzi) kuhusiana na hilo baada ya kupata barua GSM.” Juzi TFF ilitoa taarifa
kuwa, Februari 7, mwaka huu walipokea barua ya kuvunja mkataba wa udhamini mwenza wa Ligi Kuu Bara
ya NBC kutoka Kampuni ya GSM, hivyo Shirikisho hilo linafanyia kazi barua hiyo na litatoa taarifa kwa wadau.
 
Back
Top Bottom