Miaka nenda rudi Njia ya Dar es Salaam - Mbeya ndio imekuwa njia ambayo ni gumzo kwa mabasi yake kwenda mbio.
Umbali wa safari ni zaidi ya kilometre 800, na njia imekuwa ikipita kwenye Milima mikali, kona kali, mbuga ya wanyama, hali ngumu ya hewa Ikiwa ni Pamela na uwepo wa ukungu mzito na upepo Mkali.
View attachment 1879605
Hiyo ndio njia ya Dar Es Salaam- Mbeya ilivyo.
Na uwepo wa changamoto hizo Kuna wanyama wenye miili ya watu, wakikakaa Kwenye usukani wao wanawaza jambo Moja tu, nitawafikishaje abiria mapema na salama.
View attachment 1879606
Hapo ndipo unapokutana na ligi ngumu isiyo rasmi kati ya kampuni mbili, Golden Deer (New Force) na Sauli a.k.a Mnyama Mkali.
Golden Deer wao wakitumia mabasi ya kutoka China na Sauli wakitumia mabasi ya Ulaya, Ujerumani na Sweden. Sauli wana Mercedes Benz na Scania na Golden Deer wakitumia Zong Tong Climber.
View attachment 1879608
Magari haya yametengeneza mashabiki wengi huku mashabiki wao wakijigawa upande mmoja na mwingine, na askari pia wana timu zao kwenye ligi hii.
View attachment 1879609
Mwendokasi ni Hatari kwa usalama na maisha ya abiria, watumiaji wengine wa Barabara, mazingira na hata vyombo vyenyewe.