Ligi Kuu Tanzania Bara, Februari 16, 2019: Kariakoo Derby, Yanga SC 0 - 1 Simba SC

Ligi Kuu Tanzania Bara, Februari 16, 2019: Kariakoo Derby, Yanga SC 0 - 1 Simba SC

Hakika leo Yanga atakuwa kakubali kuwa Simba ni Mabingwa wa soka ndani ya mikoa 26.Tuliwaambia Yanga mpira wenu mdogo hawakusikia kama Mwarabu kapigwa itakuwa nyie? Dakika 90 SIMBA 1 YANGA 0

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bahati ilikuwa upande wako leo....ila soma ubao...
IMG_20190216_190647.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msikate tamaa wana yanga simba imewafunga kwa sababu mechi ilipangwa muda mbaya mlikuwa mnaona baridi kali sana.

Sasa mechi ijayo ongeeni na TFF ipangwe saa nane mchana mtashinda tu kwani simba kwenye jua Kali na joto Kali ni wabovu sana.

Mjipange tu.
Yanga wabishi tu Simba mpira wao mkubwa utabana mwisho utaachia tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo Yanga alikuwa nyumbani apo Taifa kafa moja bila kama alivokufa last week yule muarabu wa Shamu/Mediterania, bahati yake!! goal moja tumemstahi sana...

Simba ni at..t..areeh, AS Vita lazima afe, na yule muarab alomfukuza kocha kisa sisi atamfukuza na huyu kocha mpya

Simba taifa kubwa!
M.K 14 ni motoh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza niwapongeze watani kwa ushindi waleo ila pia nikili kwamba kama shabiki wa yanga nisingeweza kusema kwamba tutafungwa japo moyoni nilikuwa nafahamu tutafungwa kuanzia goli tatu nakuendelea.

Nipende kuwapongeza wachezaji na benchi la ufundi la timu yangu kwa kuipigania nembo ya timu kwa moyo mkubwa sana licha ya magumu tunayopitia kama timu, niwaombe mashabiki wenzangu wa yanga tuendelee kuchangia timu yetu kwa moyo mkunjufu kabisa, nivile tu uwezo wa kipesa sina kwa kiasi hicho ila ningekuwa nazo zakutosha nafikili leo ningewapa posho ya kutosha achilia mbali matokeo ya leo. Mungu ibariki yanga mungu tubariki wanayanga.
Yanga wamepambana, wmeufanya mchezo kutokua na nafasinyingi. Kwaujumla timu ilicheza vizuri kabwili hakua na kashkash Boxer amecheza vizuri alimkamata ipasavyo Okwi ila matokeo ya mpira ndivyo yalivyo Simba wamepata nafasi mbili wametumia moja. Yanga wamepata nafasi mmoja hawakuweza kuitumi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom