Ligi ya Morrison na Simba kwenye suala 'Release letter' imefikia patamu

Hawana mahusiano gani mema?
 
Kwani ile barua waliandika simba ilijielezaje? Simba si wamesema wameachana na Morrison asa kama umeshasema mmefikia makubaliano ya kuachana kwanini wasimpe talaka yake?
 
Kumpa release letter kabla ya mkataba wake kuisha ndiyo uswahili wenyewe, ambao kwasasa haupo pale Simba Sc kama ulivyokili mwenyewe.
Kujua kuwa mchezaji umetangaza kuwa mmemsimamisha mpaka mwisho wa msimu na kutakia heri katika maisha yake mapya ya soka halafu unamnyima haki ya kusajiliwa na timu zingine kisa tu muda bado wa mkataba ni uswahili zaidi.

Dirisha la CAF linafunguliwa tarehe 30 kwahiyo mpaka hapo Simba wanamkomoa Morrison asisajiliwe abakie hana timu.
 
Kweli mpira wetu kivyetu vyetu, mchezaji ambae alifanya mkaenda CAS kushtaki na kuishia kutumia gharama kubwa kuendesha case yake na mwisho wa siku akashinda Leo hii mnamtaka tena.

Waliokuwa wanaponda anachokifanya Yanga ndio wale wale ambao leo wanaponda anachokifanya Simba, kilichobadilika ni hisia na mihemko tu.

Morrison hajaachwa na Simba, bali alipewa likizo na club Kwa ajili ya kwenda kumaliza matatizo ya kifamilia, ni wazi kuwa Simba walijua next move ya Morrison ni ipi hivyo hawakuwa na haraka nae hata kidogo wakawa wanasubiri wakati kama huu ufike.

Wanachokifanya Simba ndio ambacho kingefanywa na club yoyote ile, unatoa release latter pale ambapo kuna mawasiliano mazuri Kati ya mchezaji/club inayomtaka, sasa Yanga wao wamekaa kimya tu wamemwachia hii issue Morrison.

Yanga ndio walipaswa kuongea na Simba kama wao ndio wanamtaka Morrison ili Ku speed up mchakato wao, kwani Simba wao wanaendelea kumlipa Morrison kama mchezaji wao, kwahiyo habari za kutoa tu release latter kienyeji enyeji huo ndio uswahili sasa.

Kwenye issue ya Morrison Yanga walizamilia kuikomoa Simba tangu mapema sana ndomana wao wakakubali kuingia gharama za kuendesha case CAS ilhali wangeweza kusubiri mkataba uishe kisha kumrudisha mchezaji wao, Morrison kafanikiwa kucheza na Akili za viongozi wa hizi team mbili.
 
Hawakusema wamemsimamisha, walisema wamempa mapumziko mpaka mwishoni mwa msimu
 
Hapo wanamkomoa mchezaji coz hao Yanga hata bila BM3 bado watafanya vizuri zaidi
 
Maana yake timu nyingi ambazo zinacheza champions league haziwezi kumsajili kwa kuogopa kutomtumia huko, maana yake anakosa timu za maana kuchezea hapa Afrika.

Huko ni kumkomoa mchezaji ambaye alitumia jasho na damu ktk kuichezea timu yako na kwasasa kama hauna matumizi yake hauna haja ya kuziba riziki yake
 
Yanga watalipa fine ya kuchelewesha jina la Morrison CAF ila atakipiga bila wasiwasi.Wanachokifanya Simba ni uswahili wa kawaida wa vilabu vyetu, especially wao ni mbumbumbu fc Kwaiyo wako sawa.
Deadline haina fine mkuu...
 
Daaaah sema ile barua ya kumtakia mapumziko mema ndo inaanza kufumbua macho [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] madam aliupigaa mwingi
Yaaah ni kawaida kwa wanawake kuwa na tabia ya sitaki nataka nyingi

Wanawake huwa hawaeleweki siku zote wanachokitaka
 
Reactions: Lee
Katika mazingira ya kawaida Benard angeweza kuununua mkataba wake, lamini kwakuwa simba na Benard hawaelewani na bernad anataka kwenda yanga, basi simba hawatakubali aununue mkataba bali ije timu inayomtaka ili inunue huo mkataba.
 
Hawakusema wamemsimamisha, walisema wamempa mapumziko mpaka mwishoni mwa msimu
Kwahiyo kwa kauli hiyo, je wamekaa mezani kuongeza mkataba ili ithibitishe kuwa hawakuachana bali kapewa mapumziko pekee?

Kama hatokuwa sehemu ya kikosi msimu ujao halafu hawampi barua ya kuachana nae au hata kumwita juu ya kukubaliana kuhusu kusitisha mkataba kwa makubaliano ya pande zote mbili ni uhuni unaofanywa na Simba kumpiga pin asicheze tena mpira msimu ujao
 
Hapo wanamkomoa mchezaji coz hao Yanga hata bila BM3 bado watafanya vizuri zaidi
Ila yanga wangeliachanalo huyu ili afundishwe na dunia. Watafute mchezaji zaidi ya Morrison kwanini nguvu nyingi inatumika kwa huyu mchezaji utafikiri yupo pekee yake Africa nzima
 
Kumbe kusimamia sheria sikuhizi ni uswahili? Basi uswahili hautakaa uishe duniani hapa.

Hakuna upumbavu kufanya mambo kwa hisia wakati mwanzoni yalifanyika kisheria, kibyovyote vile Simba Sc ni lazima wahakikishe hakuna mlango wa kuja kusurubiwa na BM3 kama jinsi ambayo aliwafanya Yanga Sc.

Ili uone uzito wa hili swala, basi unapozungumzia hii issue, usisahau uhusiano mbovu uliopo kati ya Simba sc na yanga , lakini pia zingatia tabia husika ya mlengwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…