Anayekomolewa hapa ni Morrison, nakumbuka kuna ishu ilitokea zamani kati ya Yanga nadhani na Dante. Yanga hawakumuingeza mkataba Dante wakawa wanapigana danadana tu na hawakusema kama hatutokuongezea mkataba. Hivyo akajikuta mkataba umeisha na dirisha la usajili limeshafungwa. Hili litatokea kwa Morrison, dirisha la usajili CAF limebakiza siku tisa tu lifungwe. Bila shaka mkataba wa Morrison unatamatika na sijui kama wamekaa mezani kwaajili ya kuongeza mkataba. Kama haijafanyika hilo, maanake huenda Morrison akakosa timu ya kuchezea mashindano ya kimataifa.