Ligi ya Morrison na Simba kwenye suala 'Release letter' imefikia patamu

Ligi ya Morrison na Simba kwenye suala 'Release letter' imefikia patamu

Shirikisho la soka Afrika (CAF) linatoa nafasi ya kusajili wachezaji wa kigeni hata kama dirisha la usajili limefungwa.

Kwa mujibu wa kanuni za (CAF) za usajili, baada ya dirisha la usajili kufungwa (CAF) inatoa siku (12) kukamilisha usajili, lakini unapaswa kulipa faini ya USD $ 5000/=.

$ 5,000. ni sawa na Tsh 11 Milioni.
 
Mm siwajali Utopolo. Nachojali ni maslahi ya Simba. KAMA HATUMTAKI, HATUMTUMII TUNAMSHIKILIA WA NN? KWA FAIDA GANI?
Jamaa mkataba wake si bado haujaisha,kwa akili zake Morrisson ukakaa nae chini ukisitisha mkataba wake huko mbeleni anaweza kukushinda na ukamlipa yeye,Mapungufu ya kisheria waliyoyafanyaga Yanga yaliwagharimu kama ivyo wakajikuta wanapeleka kesi Cas,
 
Kuliko yanga watoe million 70 kuvunja mkataba wa Morrison pale simba uliobakiza mwezi 1 na nusu ni bora watoe million 11 CAF baada ya mkataba wa Morrison kuisha
 
Kwani wajomba.
Kwa mujibu wa CAF michuano ya hatua ya awali itaanza Mwezi wa 9.
.
Time line ya Taratibu za kuwasilisha majina ya vilabu shiriki, majina ya wachezaji watakaoshiriki michuano hio na ITC inaisha lini?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Usajili wa caf mwisho ni 30 june. Kama ikipita hiyo tarehe Morrison hajapewa release letter yake ina maana atakosa usajilo wa xaf kwenye mechi za awali za ligi ya mabingwa hatocheza
 
Simba ni timu yangu ila naomba kwenye hili niwaite WAPUMBAVU.
Mmeshashindwana na mchezaji muacheni aondoke zake mivutano ya Nini?
umesema vyema!
kipindi cha nyuma waliua mpira wa mchezaji mmoja kwanza kiongozi mwandamizi alimkula mke wake jamaa akamfumania wakakubaliana wayamalize.
baadaye huyo boss akamruka kisha.
mchezaji huyo akamwacha mke wake kisha boss akamwamwambia rafiki wa karibu na mchezaji huyo amuoe mke wa aliyeachwa na rafiki yake kisha jamaa akamnunulia gari na gari likaandikwa mke wa fulani.
kama haitoshi mke anakuja kuangalia mazoezi na gari huku mme wake wa zamani yupo na mme mpya yupo.
akaona isiwe tabu akatimkia timu jirani jamaa bila kuangalia kuwa huyu jamaa anategemea mpira kama hajira yake ya msingi wakahakikisha kafungiwa kwa kujisajiri mara mbili.
akaa benchi mwaka mzima na mpira ukaishia hapo!
 
Kujua kuwa mchezaji umetangaza kuwa mmemsimamisha mpaka mwisho wa msimu na kutakia heri katika maisha yake mapya ya soka halafu unamnyima haki ya kusajiliwa na timu zingine kisa tu muda bado wa mkataba ni uswahili zaidi. Dirisha la CAF linafunguliwa tarehe 30 kwahiyo mpaka hapo Simba wanamkomoa Morrison asisajiliwe abakie hana timu

Kama hujui Yanga ndiyo wanamkomoa Morrison kulipiza kisasi jinsi alivyowalambisha mchanga kule CAS. Yanga walianza kumchombeza arudi Kwa ahadi za fedha nyingi naye akaingia kichwa kichwa,alipojaa Haji akavujisha hiyo Siri hadi ikaufikia uongozi wa Simba,nao Simba wakapiga kimya tu hadi yeye . mwenyewe alipoanza usumbufu kuwa anataka kwenda kwao kutatua matatizo ya kifamilia ndiyo uongozi kiroho safi wakampa ruhusa hadi mwisho wa msimu. Morrison hakwenda kwao akabaki hapa akihifadhiwa na Yanga na ndipo Haji kwa mara nyingine tena akavujisha taarifa kuwa biashara imeshafanyika bado utambulisho tu. Huu mkakati umesukwa kibingwa sana kiasi kuwa Morrison mwenyewe hakustuka kuwa anakaangwa. Habari ndiyo hiyo.
 
🔖 Klabu ya Simba SC inataka Tsh 70 Milioni kuvunja mkataba wa Bernard Morrison wa mwezi mmoja na nusu uliosalia.

Mkataba wa Bernard Morrison katika klabu ya Simba SC unamalizika August 14/2022.

"Bernard Morrison bado ni mchezaji wetu mpaka mkataba wake utakapomalizika. Bado tunaweza kufanya Biashara na hiyo timu itakayomuhitaji. Sisi tumempa ruhusa tu"

🔍 Murtaza Mangungu mwenyekiti wa klabu Simba SC upande wa Wanachama.
.
.
Bernard Morrison atawasili nchini wiki ijayo akitokea nchini Ghana 🇬🇭, klabu ya Simba imemtaka aripoti kambini,, BM3 amegoma.
Hapa sasa ndiyo kwenye utamu wenyewe,kama ndiyo mambo ya unyumba basi hapa ndiyo kileleni. Sitii neno tena mimi.
 
umesema vyema!
kipindi cha nyuma waliua mpira wa mchezaji mmoja kwanza kiongozi mwandamizi alimkula mke wake jamaa akamfumania wakakubaliana wayamalize.
baadaye huyo boss akamruka kisha.
mchezaji huyo akamwacha mke wake kisha boss akamwamwambia rafiki wa karibu na mchezaji huyo amuoe mke wa aliyeachwa na rafiki yake kisha jamaa akamnunulia gari na gari likaandikwa mke wa fulani.
kama haitoshi mke anakuja kuangalia mazoezi na gari huku mme wake wa zamani yupo na mme mpya yupo.
akaona isiwe tabu akatimkia timu jirani jamaa bila kuangalia kuwa huyu jamaa anategemea mpira kama hajira yake ya msingi wakahakikisha kafungiwa kwa kujisajiri mara mbili.
akaa benchi mwaka mzima na mpira ukaishia hapo!
Hizi ni stori mnasimuliana wakati mnakuna nazi.
 
Kuliko yanga watoe million 70 kuvunja mkataba wa Morrison pale simba uliobakiza mwezi 1 na nusu ni bora watoe million 11 CAF baada ya mkataba wa Morrison kuisha
Unajua huo mkataba unaisha tarehe ngapi? Viongozi wako wanajua nia yao kulipa kisasi tu Kwa Morrisons
 
Simba wasipo mpa hiyo barua ya kumruhusu watakuwa wameisaidia Yanga na siyo kuwakomoa, hasara itakuwa ya Simba wenyewe na Morisson.
 
Wampe hiyo Release Letter yake aondoke nayo, ili huu ujinga wa kuimba Morisson kila siku uishe.
huo ndiyo ujinga ZAIDI. Yaani mchezaji umetumia hela kumsajili, inakulipa mshahara na stahiki zake nyingine, bado mkataba haujaisha halafu umpe barua aondoke akasajiliwe mwingine bila we kujitakia au taratibu kufuata.

Taratibu zinajulikana dunia nzima, kwamba unatuma ofa mnakaa mezani mnakubaliana.

Mbona kwa Bwalya imewezekana? Kuna tatizo gani kwa Morrison?
 
Aaghh! Huwa inachosha sana kila wakati hasa hizi nyakati za usajili anazungumziwa mchezaji mmoja tu. 😏
 
Kwani ile barua waliandika simba ilijielezaje? Simba si wamesema wameachana na Morrison asa kama umeshasema mmefikia makubaliano ya kuachana kwanini wasimpe talaka yake?View attachment 2267389
Unajua kusoma vizuri kweli? Wapi hapo wameandika kuwa wameachana? Au kumpa mapumziko ndio kuachana kwenyewe? Unaelewa kuwa mpaka sasa bado Morison anapewa stahiki zake zote kama mchezaji wa Simba Sc?
 
Kama kweli yanga wanamtaka tena huyu jamaa basi ni wajinga maradufu.
 
Kujua kuwa mchezaji umetangaza kuwa mmemsimamisha mpaka mwisho wa msimu na kutakia heri katika maisha yake mapya ya soka halafu unamnyima haki ya kusajiliwa na timu zingine kisa tu muda bado wa mkataba ni uswahili zaidi. Dirisha la CAF linafunguliwa tarehe 30 kwahiyo mpaka hapo Simba wanamkomoa Morrison asisajiliwe abakie hana timu
Mnataka awageuke Simba kama alivyowageuka ninyi? Simba wana akili, wala hawana shida ya kumkomoa mtu. Yule ni wakili anajua sheria
 
Simba wasipo mpa hiyo barua ya kumruhusu watakuwa wameisaidia Yanga na siyo kuwakomoa, hasara itakuwa ya Simba wenyewe na Morisson.
Simba itapata hasara gsni hapa? Anayepata hasara ni Morrison,jambo ambalo ndiyo nia ya Yanga kulipa kisasi Kwa Morrison
 
Back
Top Bottom