Lijue kombora la Iran linalofika Israel kwa dakika 7 tu

Lijue kombora la Iran linalofika Israel kwa dakika 7 tu

Israel ni sawa na mkoa wa Tabora, inaingia mara 23 kwa nchi ya Iran

Lakini pia Israel anaingia mara 100 zaidi katika mataifa ya kiarabu yanayomzunguka na yeye ndio anaya control, akisema tulieni, inakuwa hivyo 😁😁😁
 
Sidhani kama kibaka akitokea mtaani kwenu atapigwa na mtu mmoja.
Vibaka wamelianzisha mwenyewe, yeye muungwana kajilinda tu , ila matamko kila saa
20250626_232154.jpg
 
Mimi ninachotaka walifyatue tu , sijui wanajishauri kitu gani ? Ningekua hapo iran kitengo cha kuyafyatua nisingetoa kidole kwenye kidude cha kuyafyatua mpaka mapapai ya kizayuni niyamalize.
Mna hasira si mnadai mmeshinda vita?
 
Angebonyeza ili tuone.Aache ujingaujinga wa kuhifadhi ndevu kama mtu wa kale.
Kwani unadhani ni bomu lipi lililosasambua lile handaki la kijeshi pale jirani na hospital ya soroka?

Iran ilitumia hili bomu kulipua handaki hilo bahati mbaya upepo wa lile bomu ukasababisha uharibifu kwenye majengo ya jirani ikiwemo hospital ya soroka... Wayahudi wakaanza kulalamika Iran inashambulia hospital 😃😃
 

Sajil-2: Kombora hatari la Iran linalofika Israel kwa 'dakika 7'​

a

Chanzo cha picha: Getty Images

Maelezo ya picha: Jaribio la kwanza la mafanikio la kombora hili lilifanyika mwaka 2008

Mzozo wa hivi karibuni wa kijeshi kati ya Israel na Iran umekuwa jaribio la uwezo wa mapigano wa nchi zote mbili, pamoja na silaha zao.

Wakati Iran ilipoishambulia tena Israel wiki moja na nusu iliyopita, ilidai kwa mara ya kwanza kwamba kombora la Sajil-2 la Iran lilitumika katika shambulio hilo. Hata hivyo, Israel inadai kuwa jeshi lake lilizuia shambulio la kombora la Sajil na kulinasua kwa mafanikio kwa msaada wa mfumo wa ulinzi.

Ingawa mapigano yamesimama kwa muda, kombora hili linaonekana kuwa sehemu muhimu ya nguvu ya Iran.
Walinda Mapinduzi wa Iran wamesema kuwa mashambulizi ya Jumatano ya wiki iliypita yalifanywa kama sehemu ya "Operesheni Ahadi ya Kweli 3."

Taarifa iliyotolewa na Walinda Mapinduzi ilisema kwamba "operesheni ya 12 ya kulipiza kisasi ya Operesheni Ahadi ya Kweli 3 imezinduliwa kwa kombora zito sana la masafa marefu la Sajil la hatua mbili." Taarifa hiyo, ikielezea sifa za kombora hili, inadai kwamba Sajil ni mojawapo ya silaha zenye nguvu na sahihi zaidi za kimkakati za Iran, zenye uwezo wa kuharibu malengo muhimu ya adui.

Nguvu ya Kombora la Sajil​

a

Chanzo cha picha: Getty Images

Maelezo ya picha,Kombora la Sajil lina urefu wa takriban mita 18 nalinalotumia mafuta, jambo linalolifanya kuwa hatari.

Sajil ni kombora la balistiki la masafa ya kati lenye uwezo wa kufikia maeneo lengwa hadi kilomita 2,000. Kwa masafa haya, kombora hili linaweza kulenga Mashariki yote ya Kati, ikiwemo Israel, kusini mashariki mwa Ulaya, na sehemu za Asia ya Kati, likirushwa kutoka Iran. Ikiwa litarushwa kutoka mji wa Natanz nchini Iran, linaweza kufika jiji la Tel Aviv nchini Israel kwa dakika saba tu.
Kombora lenye jina la Hajji Kassim la Iran pia ni moto wa kuotea mbali
 
Israel ni sawa na mkoa wa Tabora, inaingia mara 23 kwa nchi ya Iran

Lakini pia Israel anaingia mara 100 zaidi katika mataifa ya kiarabu yanayomzunguka na yeye ndio anaya control, akisema tulieni, inakuwa hivyo 😁😁😁
Unajua ukubwa wa mkoa wa Tabora wewe au umejiandikia tu. Ukiziunganisha nchi za Burundi na Rwanda kwa pamoja hazifiki ukubwa wa mkoa wa Tabora. Sasa kaangalie kati ya Burundi na Israel ni nchi gani kubwa.
 
Kwani unadhani ni bomu lipi lililosasambua lile handaki la kijeshi pale jirani na hospital ya soroka?

Iran ilitumia hili bomu kulipua handaki hilo bahati mbaya upepo wa lile bomu ukasababisha uharibifu kwenye majengo ya jirani ikiwemo hospital ya soroka... Wayahudi wakaanza kulalamika Iran inashambulia hospital 😃😃
🤣🤣🤣😁😁

Wayahudi wa bonyokwa wamekimbia humu ndani

Nacheka sana Kwa kweli
 
Back
Top Bottom