Lijue kombora la Iran linalofika Israel kwa dakika 7 tu

Lijue kombora la Iran linalofika Israel kwa dakika 7 tu

Tunachojua Iran kabondwa na Goliath wao Mkuu wa Majeshi masikini walitia sana huruma, wakaanza kurusha hovyp makombora ili raia wafe wakabahatisha raia 28 mmoja kati yao alikuwa kwa khofu. Hali ni mbaya sana Iran majeneza 624 viwanda vya jeshi mitambo ya neucler marigia hindustan
 
Likiwa linaenda nchi nyingine linatumia sekunde ngapi?
NB; Ndiyo maana mnapigika kwa kuiwaza Israel tu.
Israel si ndio nchi iliyokubali aridhi yake iwe eneo la Irani kutest makombola yake

Nchi nyingine hatujui
 

Sajil-2: Kombora hatari la Iran linalofika Israel kwa 'dakika 7'​

a

Chanzo cha picha: Getty Images

Maelezo ya picha: Jaribio la kwanza la mafanikio la kombora hili lilifanyika mwaka 2008

Mzozo wa hivi karibuni wa kijeshi kati ya Israel na Iran umekuwa jaribio la uwezo wa mapigano wa nchi zote mbili, pamoja na silaha zao.

Wakati Iran ilipoishambulia tena Israel wiki moja na nusu iliyopita, ilidai kwa mara ya kwanza kwamba kombora la Sajil-2 la Iran lilitumika katika shambulio hilo. Hata hivyo, Israel inadai kuwa jeshi lake lilizuia shambulio la kombora la Sajil na kulinasua kwa mafanikio kwa msaada wa mfumo wa ulinzi.

Ingawa mapigano yamesimama kwa muda, kombora hili linaonekana kuwa sehemu muhimu ya nguvu ya Iran.
Walinda Mapinduzi wa Iran wamesema kuwa mashambulizi ya Jumatano ya wiki iliypita yalifanywa kama sehemu ya "Operesheni Ahadi ya Kweli 3."

Taarifa iliyotolewa na Walinda Mapinduzi ilisema kwamba "operesheni ya 12 ya kulipiza kisasi ya Operesheni Ahadi ya Kweli 3 imezinduliwa kwa kombora zito sana la masafa marefu la Sajil la hatua mbili." Taarifa hiyo, ikielezea sifa za kombora hili, inadai kwamba Sajil ni mojawapo ya silaha zenye nguvu na sahihi zaidi za kimkakati za Iran, zenye uwezo wa kuharibu malengo muhimu ya adui.

Nguvu ya Kombora la Sajil​

a

Chanzo cha picha: Getty Images

Maelezo ya picha,Kombora la Sajil lina urefu wa takriban mita 18 nalinalotumia mafuta, jambo linalolifanya kuwa hatari.

Sajil ni kombora la balistiki la masafa ya kati lenye uwezo wa kufikia maeneo lengwa hadi kilomita 2,000. Kwa masafa haya, kombora hili linaweza kulenga Mashariki yote ya Kati, ikiwemo Israel, kusini mashariki mwa Ulaya, na sehemu za Asia ya Kati, likirushwa kutoka Iran. Ikiwa litarushwa kutoka mji wa Natanz nchini Iran, linaweza kufika jiji la Tel Aviv nchini Israel kwa dakika saba tu.
Muda hausaidii kitu kama halilengi target. Mwenzao amewatarget viongozi wote waandamizi na wametangulia mbele, bila kujali muda
 
Back
Top Bottom