Likizo kwa wanafunzi iwe ni lazima

Wazo lao ni zuri sana lakini lingekuwa zuri zaidi kama wangetuboreshea mazingira kwanza ili na sisi kina kabwela watoto wapate elimu bora kama viongozi wetu huko juu ambao licha ya kukataza tuition huwezi amini watoto wao wanafuatwa na walimu majumbani kwao kufundishwa!

Hata walimu wanahitaji kupumzika pia kama wanafunzi lakini watuboreshee mazingira!
 
Mimi nimefundisha shule za serikali , lakini sikusoma hizo shule , niseme tu Agizo la Mh Waziri ni siasa.... Tupu na leo nilikuwa nanunua maandazi hapa uswahilini nimeshangaa kuona wazazi wanafurahia hili tamko la kisiasa .


Shule za serikali ili Mwanao afanye vizuri muache Wakati wa likizo aendelee kusoma maana shuleni kunakuaga na utulivu Mkubwa wa kifikra na ufahamu na. Idadi ya Wanafunzi inakua ni ndogo.
 
Nashanga lile agizo limetenguliwa ... La watoto kutobaki shuleni waende likizo. Sijui ni Nani yuko nyuma ya hiki...
 
Walimu shule za serikali inajulikana hawajali mtoto wa mtu. Amalize sylabus au asimalize no one cares!
 
Mwalimu mie nadhani suluhisho ni kuwa na specialization toka umri wa awali kabisa wa mwanafunzi!
Mtoto wa primary ana masomo zaidi ya nane hii leo, halafu akifika advance ndo anapata option ya kuchagua matatu!! Kwa nini asiwe na masomo hayo matatu toka awali ili amalize sylabus mapema?
 
Kuna katoto Cha kidato Cha 4 namsubiri kwa shauku kubwa, nikafundishe biology ya pre form five. SoMo la uzalishaji. 😁😄
 
wapi umeona nimelalamika mtoto wangu kubaki shule wakati wa likizo.? au nilikuwa namwambia mtoa mada kuwa hicho anachokitaka hakiwezi kumsaidia kitu labda angeomba mfumo mzima wa elimu ubadilishwe. usipopambana na mtoto wako hakuna waziri au mbunge wa kuamua future ya mtoto wako ndo maana watoto wao utawakuta international school wakipambania future zao waje kulamba asali kama baba zao sasa wewe maskini endelea kuwalilia badala ya kupambana na mtoto wako ukitaka awe mcheza mpira , mfanya biashara mkubwa,msomi wa maana lazima upambane kuanzia chini sio kulilia walamba asali wafanye maamuzi juu ya kizazi chako.kuzaliwa maskini sio tatizo ila kufa maskini ni tatizo.Ni sawa na mwanamke anaechezea kichapo kila siku kutoka kwa mume wake anaomba serikali ije kumsaidia sasa hizo ni akili au matope.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…