chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Kuondoa ujinga ni dhana Pana, haimaanishi kujua kusoma na kuandika tu ndio kuondoa ujinga. Moja kati ya fursa tuliyoipata katika awamu ya tano, ni kujua kwamba, kama taifa, tuna kundi kubwa sana la wajinga, ambalo, limekaa pale, linasubiri mtu alitumie tu, na litampa uhalali wa kutenda maovu makuu ya kuchukiza, ya kihayawani, na ya makufuru. Lakini, maovu hayo yatakuwa na uhalali wa sanduku la kura, kama ilivyokuwa kwa Hitler, na yeye alishinda kwa kura nyingi. Muovu ana uhalali wa kura! Hivyo ni kiongozi halali kikatiba!
Tuna kundi kubwa lililosherehekea utekwaji, mauaji, ukatili, kubambika kesi, kunyanyasa watumishi, dhuluma kwa wafanyabiashara, kundi Hilo kubwa ni la JPM.
Kama taifa, lazima tuwe na mikakati ya kuondoa ujinga katika kundi hili. Ujinga wa kuwafanya waelewe kwamba yale yalikuwa ni matendo ya kihayawani kabisa na hayafai katika nchi hii.
Fikiria mhitimu wa chuo kikuu asiye na ajira aliyekuwa anashangilia JPM kuzuia ajira serikalini na kuua uwezo wa sekta binafsi kuajiri.
Muajiriwa wa mfanyabiashara anafurahia uonevu dhidi ya bosi wake, baada ya mwezi kampuni inakufa, anakosa ajira
Fikiria mkulima wa korosho, mnazi mkubwa wa JPM japo aliona zao la korosho lilivyonajisiwa.
Tafakari mwananchi anayesifu sera za kunyima watumishi maslahi, halafu anaishi kwa kutegemea ndugu zake ambao ni watumishi ... Kila siku kupiga mizinga.
Fikiria watanzania waliokuwa wanashangilia kwa furaha kubwa kuona au kusikia fulani katekwa, mfanya biashara fulani kafilisiwa au kabambikwa mamia ya kesi, au kanyanganywa fedha zake zikizokuwa benki.
Mkuu wa Mkoa anaiba au kudhukumu magari, halafu anayawekea plate number za serikali, na like kundi la wajinga linatopea katika kumsifu sana kwamba ni kiongozi bora,gari ya wizi anaweka plate number za Mkuu wa Mkoa (RC)!
Nadhani kama nchi, tuandae programu maalum ya kuufuta ujinga huu ili kundi hili kubwa la wajinga,lipate uelewa. Haijalishi ni shilingi ngapi itatumika, lakini taifa litaponywa.
Kundi hili bado lipo, lina kiu ya damu ya watanzania wenzetu na halijashiba, ilibidi wengine wafukuziliwe Malawi, maana muda wote walikuwa wanaimba damu! Damu! Damu!.
Tutumie Redio,tv, na wasanii, shule, vyuo, viongozi katika hotuba kuufuta ujinga huu. Kila kiongozi akipata fursa ya hotuba aseme hili.
Kundi hili linahitaji elimu tu na uwazi wa taarifa ili kulivua utando wa propaganda za kipumbavu na kijinga kutoka awamu ya tano.
Kundi hili yule aliyefukuziliwa Malawi alikuwa anahangaika kuliweka pamoja ili limpe kura, jitihada zifanywe kuibomoa gundi iliyolishikamanisha, viongozi wanaoendelea kulitegemea ili wapate kura, wabomolewe kisiasa kabla hawajabomoa taifa.
Mama Samia amefanya makubwa sana kulijenga taifa na kulifanya liwe pamoja ...tumuunge mkono kwa namna yoyote ile