Lililokuwa taifa la kupigiwa Mfano halipo tena

Bashiru, Kabudi, Slaa, Mkumbo wako wapi? tunaolalamika ni wale ambao tupo mbali na huu mfumo ovu wa kuiba pesa umma, hata wewe leo ukiteuliwa utaanza kuiba mapambio pekee.

Wengine tunawanyooshea vidole walioliuwa taifa kwa ubinafsi wao.

Leo hii hata ubakaji na ulawiti wa watoto unaousikia kwetu, ni matokeo ya kufa kwa uthubutu wa kuhoji.



Tambua kwa msimamo huu wa Nyerere wenye nchi ni wananchi. Nani atalialia? Nani atakuwa Mungu mtu?

Zingatia mada mjomba kujipambanua unaishi zama zipi.
 

Si kweli kuwa mwalimu hakupenda kuhojiwa. Msimamo wa Nyerere kuhusiana na hoja tofauti ulikuwa ni huu:



Nyerere hakuwa na taabu na wenye hoja bali wenye kutaka kulpua mlang.bila kujali waliomo.

Nikuulize kuutathmini msimamo huo kabla ya ku draw conclusion.
 
Reactions: Ame

Kufa kwa uthubutu wa kuhoji huzaa miungu watu. umeshindwa kujibu hata swali hili:

Kwanini Uzi kumhusu mjumbe huyu BAK ulifungwa?


Kwanini kusiwepo uwazi na Ukweli kwenye mambo yote?

Kumhoji awaye yote ni haki yetu.

Tuseme hapana kwa miungu watu.
 

Kama nawaona johnthebaptist, Sexless, Pascal Mayalla na wenzao wakipita juu kwa juu kimya kimya.

Sana sana wakijisemea: hiiiiiiiiii!

Si mbaya wandugu tukawa wa wazi tu.

Hamjambo lakini kukote Kule mlipo?
 
Watanganyika wa kawaida ni watu wema wakarimu na hawana ubaguzi. Nenda popote, utake kuishi, biashara, utangaze dini, uoe au uolewe n.k utakaribishwa. Hii ni fursa kubwa sana mtu kutafuta maendeleo.
Ni kundi dogo sana lenye nguvu ya uhodhi lenye jeuri ya kulinda wanachotamani.
Wapo wanaopigania kuingia huko lakini wanakabiliana na shida ya mwenye nguvu mpishe.
Watu wa kawaida ni wengi sana, wana meno lakini wanaogopa kung'ata sababu kuna mishale imelengwa.
Tanzania kwetu pazuri.
 
Na kwa maelfu ya wazee na ndugu zetu waliouliwa kwa uvamizi wa Nyerere , Zanzibar , na kwa kuidanganya dunia kuwa nchi zimeungana na kuibadilsha Tanganyika na kuiita Tanzania
 
Watanganyika wale kabla ya uvamizi lakini hawa walionyeshwa sumu ya ubaguzi na Nyerere ni shida sana
 
Nyerere alikuwa na uwezo wa kufuta vyama vya upinzani wakati wa kupigania uhuru?
 
Mzee ana miaka 96 ameshazeeka, ni somo kwa wanasiasa vijana juu ya kujishusha na kukubali kukosolewa.
 
Mtutuwandei.

Nyerere aliviunganisha vyama vya siasa, na kwa kuviunganisha kwake, ni sawa na kuvifuta vingine vilivyokuwepo kwani havikuwepo tena.
 
Kama nilivyokwambia awali, reasoning yako nimeshajua iko influenced na kitu gani, hivyo kwako sio rahisi kuona lolote zuri la Nyerere.

Hiyo mentality uliyonayo dhidi ya Nyerere na wengine wa aina yake, kuna mahali ulipandikizwa, sasa kwako kuiondoa itakuwa ni vigumu sana, naona utamtafutia Nyerere kila sababu ilimradi ujiridhishe ili kutimiza lengo lako ovu.

Kuhusu ushauri, hakuna nilipokwambia Nyerere alishauri hilo peke yake, najua walikuwepo na wengine, lakini kwa nafasi ya Nyerere huwezi kuiweka kwenye mizani moja na hao wengine, huu ndio ukweli japo najua hutaki kuusoma.

Suala la kukoswa kupinduliwa hayo yalikuwa ni maamuzi ya wachache, kwenye uongozi siku zote hayupo kiongozi wa kupendwa na wote, kama unae tuambie ni yupi? usitake kuniaminisha hayo yalikuwa ni maamuzi ya wengi, kwamba walikubaliana kumpindua kwa sababu yoyote ile.

Naamini hata leo hawa viongozi waliopo nao wangepinduliwa, kwani kiujumla hali ya maisha ya mtanzania haijabadilika kwa kiasi kikubwa kihivyo, bado ni shida tupu hasa huko vijijini na hata mijini, lakini watu tumetulia tu licha ya kero zote zilizopo.

Kuhusu yeye kuomba msaada kwanza hili nalisoma kwako; kama ni kweli, unaonesha vile ulitaka Nyerere apinduliwe ili ufurahi, you are confused mpaka unatetea uhuni.

Msaada aliuomba Uingereza kama serikali yake kwa wakati huo haikuwa na uwezo wa kuzima hayo mapinduzi, hili sio kosa, lakini hili lisingemaanisha hayo mapinduzi yangekuwa halali kama angepinduliwa kweli, na ndio maana akapewa huo msaada.

NB.
Nachojua mimi msaada aliopata Nyerere wa kuzima mapinduzi aliupata kwa Kambona aliyetumika kuwatuliza wanajeshi waasi.
 
Mie nakubali mambo mengi ya Baba wa Taifa lakini lile la detention na kukemea watu hadharani kama watoto wadogo with abusive language katu sili afiki...Yeye pia ilikuwa siyo rahisi kumwendea kwakua alikuwa mkali na hujui atakubana angle ipi, baba yangu mimi alisoma kama yeye na kwakua alikuwa anajua maana ya freedom alijiondoa mapema sana kwenye mambo haya ya kudumisha fikra hata zisizo sahihi...He trained us to be assertive na kamwe tusikubali kuwa bullied any how na mtu yeyote, jambo nililoishi nalo mpaka leo.

Kuhusu Mwl baba yetu sikuhadithiwa I had my brains wakati akifanya zile intimidations zake japo hotuba zake zinavutia...Na yeye hakukataa kwamba he had weaknesses, ni sisi tu na culture ile ile ya kujaribu kupaka rangi ukuta wenye nyufa bila kujali nyumba itaanguka ndiyo sababu mpaka leo hatutaki kutafakari yaliyo ta msingi na kutafuta dawa ya kutibu ugonjwa
 
Kanchi kananuka RUSHWA- Nyerere said in 1995.

Kama kalikuwa kananuka 1995 Hali ikoje 2022??
 
I concur with you, Tanzanians in general are very modest people, lakini mostly wanakuwa abused...
 
1961 kulikuwa na vyama vingi.
1963 sheria ya kuwa na chama kimoja ilipendekezwa.
1965 sheria ya kuwa na chama kimoja ilianza kutumika. Baada ya Uhuru kwa miaka 4
 
Yaani Nyerere angekuapo leo ngesikitika sana na yanayoendelea...na alianza kusikitika toka Mkapa alipokuwa raisi. Hata akamuuliza "unabinafsisha hata NBC kwa nini hasa? Siku moja utabinafsisha magereza"
 
Na kwa maelfu ya wazee na ndugu zetu waliouliwa kwa uvamizi wa Nyerere , Zanzibar , na kwa kuidanganya dunia kuwa nchi zimeungana na kuibadilsha Tanganyika na kuiita Tanzania
Nyerere alimuuwa nani tena Zanzibar mkuu mbona sikuelewi?
Aliwauaje uwaje? Una ushahidi wa hiki ulichoandika hapa?
 
Ndo hapo mkuu. Mwinyi ndio raisi pekee aliekubali kukosolewa na kuwasamehe wakosoaji wake. moyo huu hakuna raisi wa Tanzania aliewahi kuwa nao, hata huyo mtoto wake kule Zanzibar hawezi kufikia uvumilivu na ustahamilivu wa baba yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…