Mtu mwenye nguvu na ushawishi anakoswa koswaje kupinduliwa hadi anaomba msaada nje ya nchi (Uingereza)?
Kama angekuwa na nguvu na ushawishi huo unaofikiri basi angerudisha kwanza azimio la Arusha ambalo ndio lilikuwa jambo la muhimu na alilolipigania sana mwenyew enzi ya utawala wake.
Kuhusu ushauri sio Nyerere tu peke yake alishauri, bali hata baadhi ya wasomi, wanasheria, viongozi wa dini nk. Na kwa vile Mwinyi nae aliamini katika kukosolewa kama tulivyoona katika utawala wake basi hakuona sababu ya kukataa ushauri huo ambao yeye mwenyewe alikuwa ashaona manufaa yake ila wahafidhina wa ndan ya chama ndio waliokuwa wanajaribu kuuyumbisha yumbisha.
Kama nilivyokwambia awali, reasoning yako nimeshajua iko influenced na kitu gani, hivyo kwako sio rahisi kuona lolote zuri la Nyerere.
Hiyo mentality uliyonayo dhidi ya Nyerere na wengine wa aina yake, kuna mahali ulipandikizwa, sasa kwako kuiondoa itakuwa ni vigumu sana, naona utamtafutia Nyerere kila sababu ilimradi ujiridhishe ili kutimiza lengo lako ovu.
Kuhusu ushauri, hakuna nilipokwambia Nyerere alishauri hilo peke yake, najua walikuwepo na wengine, lakini kwa nafasi ya Nyerere huwezi kuiweka kwenye mizani moja na hao wengine, huu ndio ukweli japo najua hutaki kuusoma.
Suala la kukoswa kupinduliwa hayo yalikuwa ni maamuzi ya wachache, kwenye uongozi siku zote hayupo kiongozi wa kupendwa na wote, kama unae tuambie ni yupi? usitake kuniaminisha hayo yalikuwa ni maamuzi ya wengi, kwamba walikubaliana kumpindua kwa sababu yoyote ile.
Naamini hata leo hawa viongozi waliopo nao wangepinduliwa, kwani kiujumla hali ya maisha ya mtanzania haijabadilika kwa kiasi kikubwa kihivyo, bado ni shida tupu hasa huko vijijini na hata mijini, lakini watu tumetulia tu licha ya kero zote zilizopo.
Kuhusu yeye kuomba msaada kwanza hili nalisoma kwako; kama ni kweli, unaonesha vile ulitaka Nyerere apinduliwe ili ufurahi, you are confused mpaka unatetea uhuni.
Msaada aliuomba Uingereza kama serikali yake kwa wakati huo haikuwa na uwezo wa kuzima hayo mapinduzi, hili sio kosa, lakini hili lisingemaanisha hayo mapinduzi yangekuwa halali kama angepinduliwa kweli, na ndio maana akapewa huo msaada.
NB.
Nachojua mimi msaada aliopata Nyerere wa kuzima mapinduzi aliupata kwa Kambona aliyetumika kuwatuliza wanajeshi waasi.