Limekaaje suala la madalali kulipwa kodi ya mwezi mmoja?

Akitokea mwekezaji akaanzisha mfumo mzuri wa kimtandao wa kupangisha nyumba, vyumba, warehouses nk.

Kuwe na vigezo vya kuwabaini wenye nyumba kama takwa la kujisajili.

Huu mfumo utatengenezwa kimaeneo, kwamba nikiwa singida na ninahitaji chumba arusha niwe na uwezo wa kuangalia nyumba ama vyumba vinavyopatikana katika wilaya, kata, na mitaa husika na occupancy status.

Mfumo uwe na database ya wateja wote, waliokwisha pangisha nyumba vyumba, na wale wakorofi, wenye kadhia mbalimbali wawe reported na kuwe na list ya wapangaji wakorofi wote wasiolipa na matukio mengine yasiyofaa, hii itawapa fursa wapangishaji kujua tabia ya mpangaji wake mpya kwasababu kutakuwa na records za nyumba zote alizopanga, na wenye nyumba lazima waache reviews za wapangaji wao pale wanapo hama. Unaweza kuhisi itakuwaje kama mwenye nyumba kamchafua mpangaji wake kwa maksudi ili asipokelewe sehemu zingine atakazo kwenda kuomba kupanga, jibu ni kesi yoyote ya mpangaji na mpangishaji lazima iwe reported na inapothibitika mwenye nia ovu ni mpangaji basi profile yake inaweza kuwekewa nyota ndogo kuonesha yeye ni mpangaji msumbufu au asielipa kwa wakati.

Hili project inaweza kusimamiwa na serikali na itapata makusanyo mengi sana ya kodi.

Hapa madalali (kamfukoo jitegemeee)
 
Kwangu nakulipa chakunitaftia Mteja tu then sepa mazima labda km Mteja huyo aamue kuingia ubia wa kumlipa style hiyo.
 
huwa wanajiona wao ndo wamejenga nyumba ...
 
Dalali anakwambia ana nyumba ukimfuata anakwambia tumpitie mwenzangu,mkifika huko nako mnaambiwa mkampitie mwingine....nyumba ina msururu wa madalali wanne! Hapo lazima wapandishe Kodi ili ile hela ya mwezi iwakimu wote wanne.
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Yes unakuta dalali huyu uliekutana nae hana nyumba, ila mwenzake anayo so anakuunganisha nae,m kwahiyo chain ni lazima ikuumize, upo sahihi wengi wanaumizwa kwa mtindo huo
 
Madalali ni muhimu sana maana huwezi kutembea mtaa kwa mtaa kutafuta nyumba...utachukua miezi kuipata. Madalali ukitaka uone umuhimu wao uwe na bidhaa unauza au unataka kumunua hasa nyumba au kiwanja. Nadhani tuendelee kuwaheshimu hawa watu
Agent ni mtu muhimu hatukatai, duniani kote agents wapo. Tunachoangalia hapa ni ukosefu wa chombo kinachowaongoza hawa watu, hakuna. Ni kama mambo yao wanajiamulia tu, kuwe na sheria za kuwalinda na kuwaongoza pia.

There's no way chumba ni 50,000Tsh, mtu analipa miezi sita 300,000Tsh then dalali achukue 50,000Tsh. Hiyo ni kama 17% ya gharama ya chumba. Kwa nini kusiwe na chombo cha kuongoza hizi kazi? Huko masokoni nao nasikia ni hivyo hivyo, wanaongozwa kwa utashi sio sheria.

Watambulike, wawe na leseni/utambulisho ya kazi lakini wawekewe sheria.
 
Kuna watu wanadharau kazi za watu.
Naona wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa chuo wanavyohangaika kupata chumba hawa madalali wanasaidia sana.
Au itokee unauza nyumba au kiwanja au gaei tuone kama utauza bila kutafuta dalali.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe unaishi wapi? Una nyumba ya kupangisha?
Mpangaji ndiyo humlipa dalali posho sawa na kodi ya mwezi mmoja.
 
Tafuta NYUMBA mwenyewe... Information is power... Yeye ana information yakukusaidia unaTAKA akupe hiyo information bure?
 

Hapana sio hivyo Mkuu ,mwenye nyumba anakula laki 3 yake kama kawaida.....Na wewe unampa dalali elfu 50 yake.
 
Ni upuuzi mtupu ambao katika Nchi nyingine haufanyiki wa kumpotezea mpangaji muda na kumuongezea gharama. Nchi nyingine nyumba zinatangazwa kwenye magazeti au online na kodi, location ya nyumba na phone number ya mwenye nyumba huwekwa hadharani.
Wewe ni nani hadi uropoke kwamba hili halinihusu? 😳😳😳
Acha ujinga wako wa kuwaamulia watu nini kinawahusu au hakiwahusu
Biashara ya Mwenyenyumba na Dalali haikuhusu Mpangaji.
Bishara iliyopo iwapo umemtafuta Dalali ni kati yako na huyo Dalali.
Acha kuingilia yasiyokuhusu.
Na ukiona vipi achana na Dalali,
Tafuta mwenyewe,
Simple as that.
 
Sasa nyumba unaTAKA information huna...dalali hUtaki kulipa..
Waja wanna mambo
Sio kila mchangiaji kwenye uzi fulani basi anakua anakubaliana, najua ugumu wakutafuta nyumba bila dalali, mimi kipindi natafuta nyumba huwa natembea nao tunawekeana malengo anipitishe kwenye nyumba kama tano kwa siku na nachagua ni eneo gani na siku ya mwisho namtoa hela vocha elfu 5,ndani ya week lazima upate nyumba then kwenye kulipana inategemeana sasa na nyumba inapngishwa kiasi gani yani hili swala ni maongezi tu sio lazama mfuate kanuni,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…