Limekaaje suala la madalali kulipwa kodi ya mwezi mmoja?

Mimi...wakati naishi DSM...nikitafuta nyumba na dalali Nampa hela Yake bika hiyana...

Au nampa nusu nusu kila nikipata mshahara ndani ya miezi miwili namaliza deni
 

Wataalamu wa computer fursa hiyo, changamkieni fursa hiyo.

Njooni ni kitu kama Airbnb app, ambayo itwakutanisha wenye nyumba na watafuta nyumba kisha ninyi mtafaidika na waweka matangazo ya biashara.

Changamkieni fursa tuwaondoe hawa wapuuzi kama ilivyo kwa mabasi.
 
Mimi...wakati naishi DSM...nikitafuta nyumba na dalali Nampa hela Yake bika hiyana...

Au nampa nusu nusu kila nikipata mshahara ndani ya miezi miwili namaliza deni

Ni mpangilio tu cha msingi apate chochote kitu,
 
Ni matapeli tu hawa wanaohusika sana katika kuongeza gharama za kupanga nyumba/chumba. Hawataki kufanya kazi za maana bali kusubiri mteremko.,
 
Nashukuru Mungu nimepata kibanda changu na nimehamia sa hivi mambo ya Madalali wa nyumba nitayasikia kwenye Bomba tu.
Kupata kibanda chako siyo sababu ya kutoona tatizo linalowakabali wale wasio na nyumba. Nadhani hata serikali haifuatilii hili tatizo kwa sababu viongozi wengi hawakumbani na hili tatizo.
 
Dalali anakwambia ana nyumba ukimfuata anakwambia tumpitie mwenzangu,mkifika huko nako mnaambiwa mkampitie mwingine....nyumba ina msururu wa madalali wanne! Hapo lazima wapandishe Kodi ili ile hela ya mwezi iwakimu wote wanne.
Kimsingi udalali wa kwenye kupangisha nyumba siyo mbaya ila Bongo unafanyika kienyeji na kitapeli sana sana. Tatizo ni serikali hasa serikali za mitaa. Wangeweza kuweka mfumo maalum kwa kukutanisha wenye nyumba na wapangaji kwa njia rahisi, inayoeleweka na ya kistaarabu na kwa ada nzuri.
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Yes unakuta dalali huyu uliekutana nae hana nyumba, ila mwenzake anayo so anakuunganisha nae,m kwahiyo chain ni lazima ikuumize, upo sahihi wengi wanaumizwa kwa mtindo huo
Unakuta mpaka kiatu kimeisha upande lakini kwenye nyumba za watu utazani yeye ndiye mwenye nyumba, bei anapandisha yeye wezi wakubwa wale watu
 
Dodoma Ndiyo Bhalaa!!
Chumba Kipo Eti Hupewi Mpaka Dalali
 
Dodoma Ndiyo Bhalaa!!
Chumba Kipo Eti Hupewi Mpaka Dalali
Siyo Dodoma ni maeneo mengi. Ndio ujue kuwa kazi yao ni muhimu maana wao ndio wanakuwa kama wadhamini wako kwa mwenye nyumba. Ukienda ukavurunda alipokupangisha dalali ndiye atapewa lawama kwanza
 
Hao jamaa siwakubali wapuuzi sana, wanataka hela kubwa kwa blah blah let say room kwa mwezi 100 eti nayeye anataka 100K ukimpa hata 50K anakomaa kama vile kuna kazi ya maana kafanya. Nishajua dawa yao
 
Unakuta mpaka kiatu kimeisha upande lakini kwenye nyumba za watu utazani yeye ndiye mwenye nyumba, bei anapandisha yeye wezi wakubwa wale watu
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Mkuu nimecheka
 
Swala linaniuma hili jamani khaaa, yaani dalali nilimpa sh 50 elfu yangu mpaka leo inaniuma jamani khaaaaa
 
Kuna magroup ya facebook CHAMA CHA WAPANGAJI TZ jiunge humo unasahau dalali
 
Kwa swala hili nadhani tulalamike pia ada za shule kulipwa kwa Mwaka au kwa terms badala ya kwa mwezi.
 
Madalali Wana umuhimu mkubwa pia katika haya maisha! Wanasaidia na kurahisisha maisha Sana tu ila tatizo ni hiyo Kodi ya mwezi mmoja Basi!!! Kwani lazma iwe Kodi ya mwezi?
 
Jombaa yaonekana una Hasira balaa.

Chukua Kidonge cha utulivu;
Kwanza, hii ni Tanzania sio ze-ugaibuniz😅
Pili, mimi ni dalalitz, ninayo mamlaka ya kukuambia kuwa yapo yakukuhusu na yapo yasiyokuhusu pia kwa muktadha wa iwapo umemtafuta Dalali, -Sawasawa?

Tatu: Wazazi wangu walikuwa wastaarabu sana,Hawakunifunza kutusi watu.
Lakini haya Maisha sheeeeenzy sana,
Yamenikutanisha na Mahayawani mithili yako, yanayonilazimisha nitoe matusi.
FYI ninao ufaulu mzuri tu katika matusi sasa wewe jichanganye Nyau wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…