DOKEZO Limeshafika ghorofa ya 13 na linaendelea, lakini nguzo kama njiti za kiberiti

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu mie sijakuelewa, umechukizwa na jamaa kusema au nini kinatatiza hapo? Naona ni sahihi kabisa jamaa kutoa onyo, tunaona madudu mangapi kwenye miundombinu inapigwa tikitaka juu kwa juu yakitokea ya kutokea unakua msiba wa taifa. Komaa hapo hapo mtoa taarifa. Ujumbe utafika tu.
 
Mkuu, fanya issue zako, mambo ya watu achana nayo, unaweza ukawa na very limited facts kwenye hilo jambo
Mtoa mada kaandika point sana. Madhara aliyoeleza yaliwahi kutokea siku za nyuma na kumbukumbu bado zipo.
Yeye hajalalamika mtu kujenga mjengo wake isipokuwa namna lilivyojengwa ndiyo katia shaka.
Haya ya kusema afuate ishu zake na wakati mazingira anayoishi kuna sehemu panatia shaka ni ubinafsi uliopitiliza.
 
Sawa, ngoja wahusika wakajiridhishe na hayo.
 
Mimi siko hapa kulaumu mtu au kusema huyu anamakosa, point is, ujenzi unatia shaka, wahusika wakajiridhishe.
Majengo yanapojengwa huwa kuna wahusika kutoka katika authorities wanapita kufanya ukaguzi ili kuhakikisha usalama kwa wafanyakazi na kile kinachofanyika site kinakubalika. Sidhani kama mpaka hilo jengo linafika hatua hiyo wahusika hawajafika kukagua
 
Kwani kila anaekagua ni lazima.awe mwadilifu
 
Kwenye ujanja ujanja hapo sawa. Ila swala la kusema kuwa nguzo ni nyembamba so zinaweza kufail performance sidhani kama ni judgment nzuri.
 
Haya mambo hayafanywi kienyeji enyeji tu. Lazima mtu awe na permit na authorization kutoka kwa mamlaka husika; na engineer anakuwa ame approve michoro ya hilo jengo kuwa ujenzi huo ni salama. Kama hujui kitu unauliza ufahamishwe...

Mchana mwema!
Hayapaswi kufanywa kienyeji.., ila reality kuna developers sio waaminifu na wana-cut corners sio Africa tu hata UK England yaliwakuta kipindi kile jengo kuungua moto, halmashauri ilifanya uzembe wa kutumia materials zenye walakini...
 
Kwa muonekano wa hzo nguzo ilitakiwa mwisho wa ghorofa 7 tu [emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]
 
Sidhani kama wanaweza kujenga jengo LA gharama kubwa kama hilo kwa wataalam wa kuokota jalalani
Kuna jengo mitaa ya kati lilidondoka na kuua watu, lilikuwa limefika ghorofa 15, kifusi chake kilimwagwa Jangwani wakati wanalifukua. Ilikuja kugundulika baadae kuwa mmiliki alipewa kibali cha ghorofa 10.
Ukijiuliza kama naye alikuwa anawekeza pesa bila kujua madhara ndipo unajua kuwa ujinga wa Watz sio vijijini tu bali ni kuanzia wasiokuwa na pesa na wenye nazo, wasiokuwa na elimu na waliosoma, wenye madaraka na makapuku.
Dhambi mbaya kabisa na inayotumaliza ni pale unapoona kitu batili kinatokea alafu unakaa pembeni na kusema 'hayanihusu'.
Mkuu FRANCIS DA DON umefanya vizuri kuleta huu mjadala hapa ili kama kuna wenye hoja za kitaalamu waziweke na kuclear doubt, huwezi jua labda ni utaalamu wa kisasa.
 
Siwezi kubeza uzi wako,,


Ila cha kusikitisha likitokea la kutokea

Hao hao wanaopinga, wata delete hizo commentz zao

[emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…