Linapokuja suala la IMANI, Waafrika wanampigania Mungu. Likija suala la Haki zao za msingi, wanamwachia Mungu awapiganie!

Kumpigania Mungu ni sisi dhidi ya sisi, kupigania haki zetu ni sisi dhidi ya dola. Dola yenye jela, polisi, magari ya washawasha, secret detention areas n.k. Lazima uwe makini inapoelekeza vita yako.​
Lakini dola pia ni sisi.

Polisi pia ni sisi.

Serikali pia ni sisi

Kwa hivyo bado ni sisi dhidi ya sisi.
 
Dini ni scam, dini ni Ukoloni, Dini ni Uzwazwa
 
Hapo ni Somalia watu wanapigania dini ye Mwenyezi Mungu harafu Mungu mwenyewe sasa kawaacha wanakongoroka😅😅
 
Hapo ni Somalia watu wanapigania dini ye Mwenyezi Mungu harafu Mungu mwenyewe sasa kawaacha wanakongoroka😅😅
Binadamu ni kiumbe mpumbavu sana kwenye maswala ya Imani.

Badala ya kutumia uwezo wake wote wa kiakili kujipambania mwenyewe, Anasubiri kiumbe cha kufikirika kiitwacho "Mungu" kije kumsaidia.
 
Sahihi, kuna watu ukiwaondolea dini wanapoteza maana na matumaini ya kuishi kabisa
Kwani kabla ya ujio wa dini watu waliwezaje kuishi?

Wahadzabe, Watindiga, Wasandawe na Bushmen huko maporini wanaishi kwa amani na furaha kabisa bila kuwa hata na dini.

Na life lao liko poa kabisa.

Sasa inashangaza kabisa mtu mwingine ambaye ukimwondolea dini hawezi kuishi.

Mtu wa namna hiyo hana utimamu wa kufikiri sawasawa.
 
Walikuwa na animistic religions
 
Dini imesaidia sana Afrika.
Ila baadhi ya taasisi ziliitumia kiwafunga badala ya kuwafungua wanadini. WATU WA IMANI WALIPOFIKA POPOTE KWENYE MQANDIKO WALILETA MAPINDUZI MAKUBWA YA KIMAADILI NA KIUCHUMI

MUSA
YUSUFU
YOSHUA
DANIEL
NEHEMIA
ESTA
YESU
MITUME
ETC
 
Wote ulio wataja hapa ni fictional characters. Wana exist vitabuni tu kwenye hadithi na masimulizi ya kale.

Hakuna uthibitisho wowote ule wa uwepo wao.

Hawana tofauti na Abunuwasi wa kwenye Hekaya za kutungwa tu.
 
Biblia inasema tafuteni nanyi mtaona,huezi achia haki Yako burebure ni akili pungufu tunaitafuta kwa bidii zote ikishindika kwa juu ya uwezo ndo tunamwachia muumbaji wa ulimwengu

We kama huamini uwapo wa Mungu nakuuona huu uumbaji tata ni matokeo ya ajali hiyo ni akili Yako TU mkuu
 
Sema dini zimedanganya sana watu kuhusu huyo Mungu
zinamuhubiri Mungu kwa kufikiri kwao ndiyo maana maudhui ya dini moja ni tofauti na nyingine
Mimi Binafsi najua Mungu yupo na Mungu huyu yuko mbali sana na dini zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…