Lindi: Askari afutwa kazi na Jeshi la Polisi kwa kumpiga risasi mwenzake wakiwa lindo

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Jeshi la Polisi mkoani Lindi, limemfuta kazi askari No.H.2324 PC Joseph kwa kosa la kumpiga risasi askari mwenzake No J.1752 PC Onesmo Joseph wakiwa lindo katika Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa kilichosababisha kifo chake akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi ACP Mtatiro Kitinkwi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake

Askari wa jeshi la polisi aliyetambulika kwa jina la PC Joseph amemuua askari mwenzake Onesmo Joseph wakiwa kwenye kazi ya kulinda tawi la benki ya CRDB wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Kamanda wa polisi mkoani Lindi amesema askari hao walikuwa wakigombania pikipiki na tayari PC Joseph amefutwa kazi na atafikishwa mahakamni muda wowote kuanzia sasa.
 
Niliwahi kukutana na askari polisi wakiwa doria na silaha zao za moto, nikawa rafiki yao na kuanza kupiga stori za maisha, wakaona nawafuatilia ghafla wakanichenjia, nikaona isiwe taabu wakanipiga risasi waje waseme tumeua jambazi lilitaka kutupokonya bunduki tukaliwahi, ukichukulia hao askari polisi walikuwa wamelewa pombe
 
Mbona taarifa haisemi nini chanzo cha kumpiga risasi askari mwenzie, au risasi ilifyatuka bahati mbaya?

Mambo yote yameelezwa kwenye PGO ndio askari aliyoyafuata maelekezo ya pgo
 
Ukiwa na imani ya Yesu kristo Mwokozi hawakupigi risasi




[emoji2]
 
Dhamira ya kumpiga risasi ni nini tofauti zao au ndio jamaa yake na Hamza huyu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…