Lindi hadi Mbeya kwa barabara kuna umbali gani?

M
Fafanua ueleweke
Lindi-Tunduru(Km337)-Songea(Km 265)-Njombe(Km 235)-Makambako(Km 60)-Mbeya(Km 185)
Makambako hadi mbeya ni km 172 na hadi uyole ni km 162
 
Naomba kuuliza kwa mwenye kujua. Ukitoka Lindi Hadi Mbeya Kwa barabara. Umbali ukoje kulinganisha na Dar Hadi Mbeya.

Hali ya barabara pia ikoje?
Niliwahi pita hiyo ruti ni mkeka na hakuna gari nyingi zaidi unakutana lori za Dangote hakikisha mafuta unajaza ya kutosha hakuna vituo vingi vya mafuta
 
Hiyo njia ya kusini si ya makorongo matupu?
Ni barabara poa tu na ni salama kuliko Dar-Mbeya.

Haina pot holes nyingi zipo za kawaida tena chache.

Ila ni ndefu sana ni kama km 1100 hivi.
 
Sijapita ila sina imani na barabara za kusini. Maana nilienda Lindi kuna sehemu nyingi sana kuna vipande vya maintenance.

Ila naamini kwakua ni barabara kuu inaweza kua mkeka mwanzo mwenga.
Ni mkeka safi tu kuliko barabara nyingi za nchi hii.
 
Ni barabara poa tu na ni salama kuliko Dar-Mbeya.

Haina pot holes nyingi zipo za kawaida tena chache.

Ila ni ndefu sana ni kama km 1100 hivi.
pia usisahau kipande cha kutoka songea to njombe kina kona kali na miinuko/mabonde ya kutosha sana inabidi awe na utulivu katika uendeshaji.
 
Kusini gani hiyo unayoisifia hivi?

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
 
Naomba kuuliza kwa mwenye kujua. Ukitoka Lindi Hadi Mbeya Kwa barabara. Umbali ukoje kulinganisha na Dar Hadi Mbeya.

Hali ya barabara pia ikoje?
Tumia cm yako mzee maswali mengine unatuchosha tu
 
Unataka kusema kama unaendesha tanker ni hatari hiko kipande??
hatari kwa kweli ila ukiwa makini unatoboa vizuri tu na kingine jiandae kukutana na new force maana madereva wake wengi wako rough sana njia hiyo.
 
Mwezi wa pili nataka kwenda songea. Ila lazima nipite mbeya kwa issu fulani ninatoka mwanza. Ni route ipi kwa gari kufika mbeya kutoka mwanza, gharama zake kutoka mwanza to mbeya na mbeya to songea.
 
Mwezi wa pili nataka kwenda songea. Ila lazima nipite mbeya kwa issu fulani ninatoka mwanza. Ni route ipi kwa gari kufika mbeya kutoka mwanza, gharama zake kutoka mwanza to mbeya na mbeya to songea.
Utapita via dodoma then iringa unaipata mbeya gharama sijajua ingia kwenye website za mabasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…