Hivi we ni wa nchi hii kweli? We kusini unakuchukuliaje, kwanini unafikiri barabara ya kusini iwe ya makorongo kwa hiyo kwa hiyo akili yako ndogo. Hiyo lami huko ulipo ilijengwa na wananchi? Acheni upumbavu kusini ni Tanzania serikali inapeleka maendeleo maeneo yote.. Kwanza ujue barabara ya kwanza ya lami ilijengwa kusini, yaani Trunk Road number one, T001 imeanzia Dar mpaka Tunduma. Barabara ya lami kutoka Makambako kupitia Njome mpaka Songea iljengwa enzi za Nyerere kabla hata lami haijafika hata Dodoma (T006). sasa hivi kuna lami tena nzuri ya kisasa. Kutoka Lindi-Masasi-Mtwara tangia kipindi cha Mkapa. Lindi-Masasi-Tunduru-Songea iko muda mrefu. Songea-Njombe-Makambako-Mbeya tangia kipindi cha baba wa Taifa.Kuna lami kutoka Songea-Mbinga-Mbamba Bay(ziwa Nyasa). Njombe-Makete
Huwezi amini kusini hata stand zao za wilaya ni za kisasa hazipo hata huko kwenu, kwa mfano wilaya ya Nanyumbu iliyoko mkoa wa Mtwara ina stand ya Kisasa eneo linaitwa Mangaka. Stand ya wilaya ya Tunduru ni ya kisasa ni wilaya chache sana ktk nchi hii inazo. Lami imefika mpaka wilaya ya Newala ambayo iko mkoa wa Mtwara, lami imefika Ruangwa ambayo iko mkoa wa Lindi.
Nyie endeleeni tu kukenua meno kama Ngedere na ujinga wenu wa kutojua nchi yenu. Katembee uijue nchi siyo unakaa nyuma ya keyboard unaandika kwa hisia tena kuwawazia wenzako mambo mabaya. Kusini mbona kuchele. Sema watu wa kusini wastaarabu sana hawana tabia za kujisifu km watu wa kanda za kaskazini(hasa wachaga) na kanda ya ziwa (hasa wasukuma). Watu wengine kweli mna upungufu wa akili, anayejenga barabara ni serikali halafu mtu anakuja hapa eti kwetu kuna lami, kuna sehemu nchi hii wanakijiji wameshawahi kuchangia kujenga lami? Serikali yetu inajenga miundo mbinu kwa uwiano mzuri.