Ushirombomoya
Member
- May 11, 2021
- 66
- 112
Binafsi ninaamini kuna nguvu kubwa inayotufanya tuwepo Dunia. Ila siamini dini hizi za kidunia ambazo kila kukicha ni malumbano ya juu ya ipi ni bora kuliko nyingine hadi mara nyingine kuleta machafuko.
Dini hizi mbili zimezifunga akili za watawaliwa hususani Nchi za Kiafrika na kuleta mpasuko na kuwafanya kuwa kituko hadi kwa wenye dini wenyewe yaani warumi na waarabu.
Sijui kwanini Waafrika tunashindwa kuelewa kuwa kipindi hicho tulikuwa na imani zetu na tulifanikiwa, wazee waliomba mvua na kupata papo hapo, maombi zao mengine yalijibiwa pia. Ukoloni ndio unatufanya tuzione dini zetu ni za kishezi na za wageni warumi na waarabu kuwa bora.
Dini hizi mbili zote zina mapungufu hakuna iliyo bora zaidi ya mwingine zote zimejikita kueneza tamaduni zao na kudidimiza matumaini ya watawaliwa kujitambua.