Atoto
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 86,410
- 169,862
pagawa Meno yanaanza kuota kati ya miezi 4-10.
#1 na 2 zinategemea sana mtoto mwenyewe pia ni kiasi gani unajishughulisha nae kama mzazi.
Wa kwangu (wa kiume pia) alianza kukataa kubebwa kwa kulazwa tangu ana miezi mitatu. Watu walikua wananiambia nisimkalishe sababu ataumia kiuno ila mi nilichofanya ni kufuata kile mtoto wangu anachotaka na sio maneno na ushauri wa watu ambao niliona utamfanya mtoto adumae kwa kumzuia kufanya yale maendeleo ambayo yeye mwenyewe anayataka na yuko tayari. Be like that, mtoto aking'ang'ania kuinuka msaidie, akitaka kukaa mtafutie pozi la kukaa, kusimama and so on.
Nimesikia sana watu wakisema watoto wa kiume wanachelewa kutembea mpaka hata mwaka na miezi 8lakini nayo sio kweli kwa 100%.
Wangu alikaa mwenyewe na miezi 6 na alianza kutembea na kitanda akiwa na miezi 8.5 (kutambaa ni kama aliruka), miezi 10 anapiga hatua mwenyewe na mwaka mmoja alikuwa anakimbia na alishaanza kuongea.
Kenyewe ni kajanja na kepesi sana ila maendeleo yake ya haraka haraka yamechangiwa sana na kaka yake (wamezidiana miaka mitatu) alimpa sana changamoto na ari ya kukua fasta ili asibaki nyuma. Pia sisi wakubwa tulikuwa hatumbebi bebi hovyo, muda wake wa kuwa macho alikuwa anapata mazoezi ya kumtosha.
Kitu kingine ambacho nimegundua huwa kinawafanya watoto wakue taratibu ni wadada wa kazi na uvivu wa wazazi. Chunguzeni wenyewe mtagundua kwamba, kwanza wadada wa kazi huwa wana-opt kumbeba mtoto mgongoni hata kama ana kazi kuliko kumweka chini kukwepa usumbufu wa mtoto. Wazazi nao, wako radhi wabebe mtoto muda mwingi kuliko kumuacha ahangaike huku na kule kwa sababu hiyo hiyo. Hata kuwaongelesha watoto, wengi wanaona ni kazi ya bure kupiga story na mtoto asiweza kujibu kitu kinachoeleweka ila hiyo ndio njia ya kumfanya mtoto ajifunze haraka.
hii ni kweli kabisa, ukipata msichana mzuri wa kazi ni raha sasa na humsaidia mtoto kukua vizuri, my csta alipata binti mzuri yaana alisababisha mtoto akawahi kuongea na hata kutembea.
alikuwa akiwa na mtoto utafikiri yupo na mtu mzima mwenzie full kupiga nae story na wanachekaa utadhani wanaelewana, muda mwingi anamfanyisha mazoezi hasa alipoanza kusimama na kutembea, na mtoto alikuwa mbishi wa kula lkn atafanya kila aina ya vituko na ubunifu ili mtoto ale, atachukua chakula cha kwanza watasumbuana hadi kinapoa anamwacha kidogo anachukua kingine tena mpaka mtoto anashiba, it was very wonderfullduuuh! ila kuwapata wa hivyo sasa ni ngumu kweli
Last edited by a moderator: