Uchaguzi 2020 Lissu aanza kutumia Chopa. Kutikisa Bagamoyo, Kibaha na Chalinze leo

Uchaguzi 2020 Lissu aanza kutumia Chopa. Kutikisa Bagamoyo, Kibaha na Chalinze leo

Kichwa kibadilishwe kisomeke

Lisu aanza safari ya maonyesho ya helikopta leo ataionyesha kibaha,bagamoyo na chalinze
 
Nikimkumbuka Kobe Bryant na Filikunjombe sishauri sana huyu Lissu atumie Chopa, not safe hasa kwa kipindi hiki
 
Tundu Antipas Lissu, Mgombea Urais kupitia CHADEMA anayeaminiwa na wengi kushinda Urais mwaka huu leo anaanza rasmi kuruka angani kwa kutumia Chopa maalum.

Baada ya mapumziko ya siku 2 mgombea huyo leo anatarajiwa kuingia mkoani Pwani kwa kishindo ambapo atafanya mikutano mikubwa ya kampeni katika miji ya Kibaha, Chalinze na Bagamoyo

Mara baada ya awamu ya kwanza kuzindua kampeni kwenye kanda zote 10 kwa sasa lengo kubwa ni kufanya mikutano mingi ya kukutana na wananchi kwa kila mkoa na kila Jimbo la Uchaguzi.

#Niyeye2020

#Niyeye

Molemo

Wakati Magufuli anaingia madarakani sukari ilikuwa kati ya 800 na 1200 Kwa Kilo Moja. Mwaka 2016, Magufuli akaingilia Biashara ya sukari na sukari ikapanda hadi 2400.

Mwaka 2016 Magufuli alisema Matajiri wataishi kama Mashetani...alidhamiria watanzania wakose pesa, na hakusema masikini wataishi kama malaika
. Akafanya matendo makuu ya bomoa bomoa kimara bila fidia, akapora fedha za wafanyabishara za Bureu De Change, maelfu ya wafanyakazi wakakosa ajira. Mpaka leo Magufuli hajatoa riporti kwa umma kuwa ni pesa kiasi gani alichukua?


Ukiangalia mikoa Pwani, Kibaha, Chalinze, etc...Sukari ni muhimu na kipato ni kidogo.

Angalia sukari ya Malawi, Brazil, Thailand ni rahisi kuliko ya Tanzania. Why..Mfumo wa kodi ni mbovu

Burundi na Rwanda kuagiza gari ni rahisi zaidi kuliko Tanzania, wakati magari yao yanapita bandari ya Dar es salaam.

Pia ukiangalia Ngome za CCM Chalinze, Morogoro Dodoma, Shinyanga, .., nyumba za tembe ni nyingi...Gharama za ujenzi ni kubwa mno. Cementi ni ghali sana... Hakuna sababu cementi kuwa ghali sana. Maana ni mali ghafi ya hapa hapa nchini...Mfano, Mtu akiagiza Cementi Pakistani, anakuja kuuza bei chini kuliko Simba au Twiga Cementi. Bado cement ya nje kuna usafirishaji, kodi ya taifa lao na VAT ya Tanzania. Kama alivyosema Mh. Tundu Lisu, kuna tatizo TRA....
 
Mngekuwa na nia ya dhati ya kuwasaidia Watanzania ingewasaidia sana, hivi mlipoingia madarakani sukari ilikua bei gani na sasa hivi ni bei gani?
Kwahiyo hunywi chai eeh🤔? Hii pesa unayotumia kununua bando, kwanini usinunue sukari..?(jokes)
 
Waoh karibu nyumbani Rais mtarajiwa.
Leo tunaanza rasmi kurusha chopa, mgombea wetu wa Urais Mhe. @tunduantiphaslissu ( 480 X 640 ).jpg
 
Lissu angekuwa hata waziri angejua uongozi sio lele mama. Uraisi sio mchezo! Hoja zake ni kuponda tu! Ina maana akibahatika kuwa raisi, nchi jirani ikimkosoa ni kuponda tu! Hatutaki shari, kapumzika usubiri kazi kulingana na fani yako
 
Back
Top Bottom