Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Katika mjadala uliofanyika katika mtandao wa clubhouse, Lissu alipata fursa ya kuongea na watanzania juu ya mambo mbalimbali ya kisiasa ya ndani ya chama chake na nje ya chama chake.
Kijana aitwaye Lumola ambaye alikuwa ni mgombea ubunge mwaka 2020 alimuuliza Lissu swali zito ambalo Lissu alilijibu kijuu juu tu huku akikacha kujibu jingine.
Lissu aliulizwa kuwa:
1. Kwa mujibu wa katiba ya chama, mamlaka ya nidhamu yako chini ya makamu mwenyekiti ambaye ndiye yeye huyohuyo Lissu kwa sasa, yeye alitumiaje fursa hiyo ya kikatiba na nguvu hizo za kikatiba kuwashughulikia wale wote ambao amewatuhumu kupokea rushwa za Abduli?
2. Pili aliulizwa kuwa kwa mujibu wa miongozo ya CHADEMA ni marufuku kwa mtu yoyote kutuhumu wenzie rushwa bila ushahidi, akaulizwa kama ushahidi anao kwa nini hajaufanyia kazi kama mnadhimu kwa mujibu wa katiba?
3. Akaulizwa kuwa kuna mtu ndani ya chama alifanya uharibifu wa mali za chama, na yeye kama kiongozi mwenye wajibu wa unadhimu amefanya nini kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA kumshughulikia?
MAJIBU YA LISSU
Lissu akajibu kuwa kwa mujibu wa katiba ya chama lazima malalamiko ya maadili ya viongozi yapelekwe kwenye kamati ya maadili na katibu mkuu ndo katibu mkuu apeleke mashitaka kwa kamati ya maadli (ambayo kwa sasa Lissu ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo).
Hata hivyo hili jibu lake lina mawenge maana yeye NDIYE ALIYETUHUMU WENZIE. Je alishitaki rasmi kwenye nggzi husika za chama ili katibu mkuu aagize uchunguzi wa tuhuma hizo?. Lissu anapaswa kuueleza umma kuwa yeye ambaye ametoa tuhuma in public kafanya jitihada gani ndani ya chama ili hao anaowatuhumu wachukuliwe hatua na kamati ya maadili?
Swali na jibu alilotoa Lissu unaweza kulisikia hapa:
View: https://www.youtube.com/watch?v=qFRhlGlAzEw