sonofobia
JF-Expert Member
- Jun 21, 2015
- 1,171
- 4,295
Lissu hapoi wala haboi, ameendelea kuipanga safu yake na jana usiku nyumbani kwake alikuwa na kikao kizito na wajumbe wa mkutano mkuu kutoka mikoa ya kanda ya ziwa ambao hawakutokea kwenye press yake kwa sababu ambazo zipo kapuni.
Awa ni wale wanaingia kama wapiga kura kwenye uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti wa chama.
Mpaka sasa hali ni mbaya kwa Mbowe ni kama uchaguzi ameshaumaliza Lissu.
Kama ambavyo chama kimekuwa kikidai haki ya kulinda kura kwenye chaguzi mbalimbali basi kambi ya Lissu nao wamejiapiza kulinda kura zao.