Akiongea katika kipindi cha Maria Sarungi Space Jana akijibu maswali mbalimbali ya washiriki wa mjadala huo, Tundu Lissu ametoa taarifa serious kidogo kuhusu Rais na nchi yetu...
Kwamba, taarifa walizonazo kwa sasa ni kuwa "
....Madam President Samia Suluhu Hassan is held hostage..." , kwamba si yeye anayeongoza nchi kwa sasa. Ameshauriwa yeye akae pembeni na swala la usalama wa nchi awaachie PM Majaliwa na waziri wa usalama, Mchengelewa washughulike nalo...
MAONI YANGU:
Kama hii ni kweli, kikatiba imekaaje? Kama Rais huyu mama kakubali ushauri huu, atakuwa anajua kweli jukumu na wajibu wake kama Rais wa nchi...? Kwanini washauri wake wakuu wamefanya hivi..? Ni kama vile amefanywa mdoli na wajanja kuuchezea kwa kutumia "udhaifu wa mwanamke" ili wafanye mambo yao..!!
Kuna possibility kubwa hili linaweza kuwa la kweli kwa kuangalia viashiria fulani fulani...
Hebu chunguzeni ziara na matukio ambayo Rais Samia Suluhu anapangiwa kushiriki kwa takribani miezi miwili iliyopita....
Ni yale ya utoto utoto tu ambayo siyo level yake kuyafanya kwani yangeweza kufanywa na wasaidizi wake kama waziri wa sekta husika, RC au DC...
Inashangaza kuwa anajihusisha ktk mambo madogo madogo mno huku akiacha kuumiza akili kushughulika na maswala serious kama vile hali ngumu ya uchumi, tozo kandamizi, hali tete na mbaya ya kisiasa na mengine mengi yanayohusu nchi na wananchi ambayo kwa sasa yanaelea elea hewani tu bila mwongozo thabiti toka kwa Rais kiongozi makini wa nchi...
Angalia matukio anayoshiriki Rais; mfano Royal Tour, kushiriki tamasha la ngoma za kienyeji Magu Mwanza nk nk ni ya kupumbaza tu, yasiyo na positive impact yoyote katika maisha ya watu kwa ujumla. Nyuma ya matukio haya lipo lengo fulani baya nyuma ya pazia. THE TIME WILL TELL...
Naweza kuamini hili la Tundu Lissu kwa 99%...