Akiongea na wananchi wa Mtwara waliokusanyika maelfu kwa maelfu kumsikiliza, Lissu amekwenda huko na ujumbe dhidi ya unyanyasaji waliofanyiwa wananchi wa huko kwenye ishu ya gesi, korosho na Mauaji ya kutisha huko Mkuranga, Kilwa na Kibiti.
Lissu amemsiliba vilivyo Rais Magufuli kutokana na namna alivyolishughuikia siuala hilo kwa namna ambayo mkulima wa korosho alinyanyasika sana, huku kukiwa na uchukuaji wa korosho kinguvu hali iliyopelekea watu kuwa na maisha magumu ya umasikini hata kufikia hatua ya kukata tamaa kuendelea na kilimo.
Lissu amelinganisha hatua za serikali za CCM kupeleka jeshi kwa watu wa kusini kama kupelekewa vita na serikali yao wenyewe!
Pia Lissu akaelezea namna serikali ya CHADEMA itakavyokuwa tofauti kwenye kuendesha nchi, ambapo serikali yao italinda Uhuru, Haki na kuleta maendeleo.
Wakati huohuo ndugu Lissu akawaeleza wananchi wa Mtwara kuwa katika mikoa ya Kusini ya maeneo ya Mkuranga, Kilwa na Kibiti kulitokea mauaji ya kutisha, watu kupotea na wngine kuchukuliwa kutoka kwenye misikiti na kwenda kuteswa. akasema, aliyekuwa Mbunge wa Kilwa mheshimiwa Bwege alimueleza Lissu kuhusu unyama na ukatili wa kutisha waiofanyiwa watu wa maeneo hayo katika kipindi cha utawala huu wa awamu ya tano!. Lissu akasema, watu waliokotwa wamekufa katika mito na fukweni mwa bahari. Lissu akasema mambo hayo yanahitaji majibu na akasema kuwa serikali ya Chadema itatawala kwa haki
Kwa taarifa zaidi mtazame hapa Chini akiwa huko Mtwara