Lissu alimshinda Mbowe kwa asilimia ndogo sana

Wenzako wamehamia Chauma, wanakula ubwabwa! Wewe unasubiri nini? Kwani lazima ateue watu mnaowataka nyinyi? Kwani hao walioteuliwa siyo wanachama wa CHADEMA?
 
Hujitambui wewe, kura chache za wajumbe tu ila wanachama wangepiga kura huyo Mbowe asingefika hata 30%. Hata yeye alikiri lissu ana wafuasi wengi ila sio wapiga kura wa mkutano mkuu!!

Chama ni wanachama sio viongozi, hao waliokimbilia CHAUMMA wana ushawishi gani? Hivi nani pale amewahi shiriki uchaguzi akashinda wa ngazi yoyote? Wote wale ni waajiriwa tu hakuna politician pale.
 
mbowe bado alihitajika chadema, alifanya kazi kubwa sana wakina lema na lissu wakarudi nchini
 
Na hiyo ndogo ni pamoja na rushwa kubwa sana kutembea na vibahasha vya kutisha,
 
Mahakama ndiyo hivyo tena imeizika chadema kabisa. NoreNoe nayo chaliii. CCM kuiondoa madarakani labda muwaombe msaada al shabab
 

..tayari Kamati Kuu ilikuwa na wajumbe wengi zaidi wanaomuunga mkono Mbowe.

..kilichokuwa kinahitajika ktk kamati kuu ni kuteua wajumbe wanaomuunga mkono TL ili kuweka uwiano.

..TL pia alimteua Catherine Ruga, ambaye alimuunga mkono Mbowe, kuwa mjumbe wa sekretariat pamoja na kwamba alishindwa katika kura.

..Tatizo sio style ya uongozi ya TL, tatizo ni baadhi ya waliokuwa wanachama kutokuamini na kuunga mkono NRNE.
 
Hatutaki Mbowe aseme chochote kuhusu CHADEMA muda wake uliisha sasa atuachie chama
 
Mimi nikisoma maandishi kama yana hila hata ujifiche vipi nitajua. Kipindi Chadema wanamgeuka Dr Slaa nilijua siasa zetu ni zaidi ya tunavyofikiri. Hata yanayoendelea Chadema sishangai ila binafsi daima nasimama na ukweli.

Najua wengi wanapata tabu aina ya usaliti na wasaliti ila mimi nilijifunza 2015 na sishangai tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…