Tajiri Tanzanite
JF-Expert Member
- Oct 23, 2016
- 2,536
- 4,621
Hapo vip!!
Nijambo la kushangaza na kuchekesha leo Tundu Lissu kumuomba Rais Samia atumie mamlaka yake kuondoa kesi inayaomkabili mbowe mahakamani.
Ni wazi Lisu amesikika akisema hii kesi ni ya kutengenezwa na hamna kesi hapo,hivyo alisikika akimuonya Zitto kabwe kutomuombea msamaha mbowe kwa Rais Kwasababu hana kosa alilolitenda,na aliona hiyo kesi mahakama yenyewe itaitupilia mbali kwa sababu haina nguvu.
Ni wazi kadri ushahidi unavyotolewa mahakamani na jamuhuri Tundu Lissu anapata majibu ya kauli zake za kisiasa dhidi ya kesi hii.
Nadhani ametumia taaluma yake na kujiridhisha yakwamba mwenyeki hachomoki..kwahiyo kaamua kuunga mkona kauli ya Zitto kabwe kumnusuru mbowe dhidi ya mkono wa sheria.
Ila pia nina neno kwa mama,kama atapokea maombi ya zito na Lisu basi tafsiri yake ni kwamba Rais anauweze wa kukanya muhimili wa mahakama...kwabusara ni bora,mahakama ipewe uhuru wake juu ya hii kesi ya mbowe...nakama atakutwa na hatia basi mama awaachie kama wafungwa wengine kwa msamaha...
Isionekana kuna watu wanaweza kutenda kosa na kwasababu ya umaarufu wake..na hawezi kufungwa na mahakama za kitanzania kwasababu ataombewa msamaha kwa rais na atetewa na wanaharakati...
Nakushauri Rais hili swala usiwe mwepesi wa kulitolea maamuzi..mwisho wa siku utatengeneza hoja na wanasiasa kukushambulia vizuri na kudhihirishia ulimwengu yakwamba wewe ndio uliyemtengenezea mbowe kesi.
Pia kumbuka jamhuru imetumia pesa nyingi katika upelelezi ya kesi hii..hizi ni kodi za wanyonge...lakini lingine utaivunja moyo jamhuru katika kufanya kazi zake.