KWELI Lissu amesema Abdul Halima Ameir (mtoto wa Rais Samia) aliwahi kutaka kumpa rushwa

KWELI Lissu amesema Abdul Halima Ameir (mtoto wa Rais Samia) aliwahi kutaka kumpa rushwa

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Salaam Wakuu,

Nimekutana na maandiko yanadai kuwa Lissu akiwa kwenye mkutano Singida alisema mtoto wa Rais Samia aitwaye Abdul aliwahi kumpelekea rushwa akamfukuza.

Je, kauli hii ni kweli?

1717866016512.png

Tunaomba mtusaidie kutafuta uhakika

---

Video 1: Lissu akiwa Mkutanoni Singida akielezea kufuatwa na Abdul


Video 2: Lissu akieleza kufuatwa na Abdul katika Spaces ya Maria Sarungi
 
Tunachokijua
Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA anaendelea na mikutano yake ya kisiasa katika mikoa mbalimbali. Leo Juni 8, 2024 Tundu Lissu amefanya mkutano wake Singida Mjini maeneo ya Stendi ya zamani.

Kumekuwa na sintofahamu juu ya kauli inayodaiwa Lissu ameitoa kwenye mkutano huo ikimhusisha mtoto wa Rais Samia kutaka kumpa Rushwa naye akakataa na kumfukuza.

Upi ukweli wa jambo hilo:
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa kauli hiyo ni ya kweli na imetolewa na Tundu Lissu leo Juni 8, 2024 akiwa kwenye mkutano mkoani Singida Tazama Video hapo juu. Akimuongelea mtoto wa Rais Samia aitwaye Abdul. Tundu Tundu Lissu anasema

Jamaa mmoja anaitwa Abdul aliletea Rushwa nyumbani kwangu nikamwambia Shenzi, Shenzi. Kahonge kwao wanaohongeka
1717869655680-png.3012149



Abdul Halim Hafidah Ameir, mtoto wa Rais Samia
Ufuatiliaji wa JC umebaini pia hii si mara ya kwanza kwa Tundu Lissu kuzungumzia suala la kutembelewa na Abdul (Mtoto wa Rais Samia), mnamo May 23, 2024 akiwa katika mjadala wa X (Twitter) ya Maria Sarungi akielezea ahadi ya Rais Samia kumlipa pesa zake za matibabu alipokutana naye Ubelgiji

Tundu Lissu anasema:

Rais Samia aliniambia nilipokutana naye Ubelgiji Februari, 2022 nimuandikie barua ya madai yangu ya matibabu, nilimuandikia barua nilipeleka mara tatu. Nilipeleka Mara ya kwanza Juni 2022 kabla sijarudi nyumbani. Karibu mwaka ukapita bila kufanyiwa kazi. Niliporudi mwaka jana Januari nikawa approached na mtu kutoka Wizara ya Fedha Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali akiniambia kwamba ameagizwa ashughulikie madai yangu anaomba nyaraka. Ikabidi niende Ubelgiji kuzifuata, nikachukua nikamletea, hiyo ilikuwa mwaka jana mwezi nimesahau.
Baada ya hapo nilitembelewa na mtu anaitwa Abdul, nafikiri mnamfahamu. Alipokuja kunitembelea akitaka tuwe marafiki nikamwambia Mama yako anilipe hela zangu, akasema mama hajapata barua yako ya madai nikamwambia hii hapa mpelekee. Kwahiyo nimepeleka mara tatu na mpaka sasa haijalipwa (Sikiliza kwenye video 2 hapo juu)
Back
Top Bottom