Uchaguzi 2020 Lissu amwambia Rais Magufuli afungulie Vyombo vya Habari ili asisumbuke kuweka bando kuwaangalia wapinzani kwenye WhatsApp

Uchaguzi 2020 Lissu amwambia Rais Magufuli afungulie Vyombo vya Habari ili asisumbuke kuweka bando kuwaangalia wapinzani kwenye WhatsApp

Mrema mwenyewe alikuwa nayo kuliko hata lowasa
Ndugu acha kumfananisha Lissu na lowassa huyu bwana ni mpinzani kweli,tena haogopi mtu,hatafuni maneno ni mkweli ni mwadilifu tofauti na lowassa aliyekuwa mwoga na mwenye doa kubwa la ufisadi,hoja tu ya ufisadi ilikuwa pigo kwa upinzani lakini watu kwa kuichoka ccm walimpa kura zaidi ya mil 6.

Ndugu huu mwaka ni tofauti lisu anauzika lisu anajiamini, ccm imechokwa na wakulima mf wa korosho,vijana hasa wahitimu vyuo, watumishi wa umma walionyanyasika miaka 5 bilakuongezwa mishahara na kudharirishwa ovyo, wafanyabiashara mpaka wengine wamejinyonga mf yule wa viroba Dodoma, ndugu ccm ijipange uchaguzi huu sio kama miaka mingine watu wanajitambua mtampinga lissu kwa hoja gani mtu makini na mwadilifu na pia yeye ni alama ya uonevu kwa kupigwa risasi za kutosha.

Pia tofauti na lowassa, lissu anakwambia hakuna kuibiwa kura.Ushauri wangu kwa chadema mwaka huu nendeni vijijini mjini tunajielewa tutawapa kura tu nendeni vijijini hata kwenye makao makuu ya kata mkaongezee tu kura ili waibe mpaka washindwe msijifurahishe na mafuriko ya mjini au gaweni timu vizuri,wengine wajikite mjini wengine vijijini.N.b mimi sina chama ila kura yangu kwa upinzani wa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kampeni bado, lowasa 2015 kura zilitosha tena sana, na ndiyo sababu ya jpm kuzuia shughuli za kisiasa maana alijua kabisa ikifika 2020 hata kuiba kura watashindwa sasa.
Lowasa angeshinda si angekua rais!? Tusubiri matokeo ya uchaguzi tuu
 
Yaan JF ndo Tv yangu saa hv familia yang yote tunaketi tunaangalia na kusoma habari humu mambo ya tv nimeachana nayo
 
Huyu Jamaa hajawai muita Mkulu Mheshimiwa,, Yeye huwa anataja jina lake kama mtu fulani tu wa kijiweni..

Confidence ya hali ya Juu sana hio.. Niyeye pekee anaeweza kuyasema hayo
Sasa hapo ndio anapokosea, huyo "Mkulu" tayari ni kiongozi wa nchi pamoja na kuwa kwa yeye ni mpinzani wake,na ni inamlazimu "aheshimu" Mamlaka aliyonayo kiutawala ili kujenga peace and harmony na kuepusha kuamsha Chuki miongoni Mwao ,kwa kuzingatia "Dhana" inayoliliwa kila siku ya "Upinzani si Uadui"ila ni utofauti ktk Itikadi na mwisho wa siku wote tuna lengo moja la kuijenga Tanzania yetu si vinginevyo!
Kinachotokea hapo kinaweza tafsiriwa zaidi kama Utovu wa Nidhamu na si Confidence.
 
Idadi ya wagombea wa CCM inashinda hao wanayo vumisha, Maelfu wampokea Lissu. Lakini kitendo cha CCM kujivunia jezi zao mtaani ni ishara nyingine awamu ya 5 kazi ccm wameifanya. Odinga hapo Kenya kuna picha ya mtandaoni kavaa shati la jezi ya CCM...
Kwahiyo unashauri anyamazishwe kama kule Dodoma? Huyu sasa ndio mzalendo na sna ujasiri ambao hakuna aliyenao huko kote mnaoimba mapambio. The guy is fearless.
 
Chadema kumbukeni mafuriko ya mzee Slaa na mzee lowassa. Lakini ccm ilishinda. Bungeni mhe Peter Msigwa alipata kusema maana ya insanity.

Wao waliongoza kipindi ambacho mikutano na siasa ilikuwa ni ruksa
 
Kwahiyo unashauri anyamazishwe kama kule Dodoma? Huyu sasa ndio mzalendo na sna ujasiri ambao hakuna aliyenao huko kote mnaoimba mapambio. The guy is fearless.

Wewe ni wa hovyo na mbinafsi kama huyo Lissu hayo Dodoma yamekujaje hapa? Hapa tunazungumzia maslahi mapana ya taifa, na kukataa viashiria vya kusambaratisha nchi hii.
 
Chadema kumbukeni mafuriko ya mzee Slaa na mzee lowassa. Lakini ccm ilishinda. Bungeni mhe Peter Msigwa alipata kusema maana ya insanity.
CCM kumbukeni kuwa kila siku mnaimba kuwa upinzani umekufa, lakini oneni watu wanavyofurika kwenye mikutano ya upinzani. Kama mnjiamini sana wekeni uwanja sawa wa kura muone moto utakavyowawakia
 
Chadema kumbukeni mafuriko ya mzee Slaa na mzee lowassa. Lakini ccm ilishinda. Bungeni mhe Peter Msigwa alipata kusema maana ya insanity.
Slaa and Lowasa wote walitoka ccm sasa hatujui kama walikuja kwa special mission wamemaliza na kurudi nyumbani, tunashukuru kutukumbusha maana ya insanity Ila jua Lissu ni kiumbe tofauti hatakubali ile michezo ya chaguzi zilizopita.
Kinachotokea Mali mnaweza ona hakiwezi kutokea hapa lakini chini ya jua hakuna linaloshindikana..
 
Hapo wameenda kumshangaa tu Ila kura ni kwa CCM .
 
Chadema kumbukeni mafuriko ya mzee Slaa na mzee lowassa. Lakini ccm ilishinda. Bungeni mhe Peter Msigwa alipata kusema maana ya insanity.
Haya ni awamu ya tano iliyofanya mambo makubwa ambayo hayajafanywa na serikali zilizopita....hv bado huoni tofauti we kiaz
 
Akiwa mjini Tunduma, Tundu Lissu katika harakati zake za kutafuta wadhamini, ameongea na maelfu ya wananchi.

Amezungumza kuhusu hali ya uminywaji wa Vyombo vya Habari nchini, watumishi wa umma kutopewa maslahi yao ipasavyo, kero za wafanyabiashara ndogondogo hususan vitambulisho vya wamachinga vya sh 20000, Viongozi wa dini ya waislamu walioko jela kinyume cha haki, uonevu dhidi ya vyama vya siasa, kero ya wafanyabiashara kubambikiziwa kodi na TRA na kusema kuwa watavikomesha hivyo october 28.

Na pia, akampiga kijembe Rais Magufuli kuwa badala ya kuhangaika kuweka bando la internet ili kuwatazama wapinzani kwenye WhatsApp, afungulie vyombo vya habari ili awaone kupitia vyombo rasmi vya habari.

Hapo Tunduma OCD wa sehemu hiyo alijaribu kuwazuia wananchi kwenda mkutanoni, lakini alishindwa kuwathibiti wananchi maana walikuwa ni wengi mno.

Kwa taarifa zaidi muone yeye mwenyewe Tundu Lissu.


Rais mtarajiwa wa wanachadema, Hoja zake hata wanachadema wenzake wanazomea wanazomea, Toka Chadema iuzwe kwa Bwana Ngoyai, Sijawahi kuhisi mwanachadema anayeweza kupewa dola.
 
Back
Top Bottom