Uchaguzi 2020 Lissu amwambia Rais Magufuli afungulie Vyombo vya Habari ili asisumbuke kuweka bando kuwaangalia wapinzani kwenye WhatsApp

Uchaguzi 2020 Lissu amwambia Rais Magufuli afungulie Vyombo vya Habari ili asisumbuke kuweka bando kuwaangalia wapinzani kwenye WhatsApp

Ilikuwa ni kosa kubwa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa kwa miaka 5. Wananchi wamekuwa kama wamefunguliwa kifungoni kwa kukosa uhuru.

Hakutakiwa kuifungia moja kwa moja alitakiwa aimanage vizuri tu na mambo yangeenda sawa
 
Wewe ni wa hovyo na mbinafsi kama huyo Lissu hayo Dodoma yamekujaje hapa? Hapa tunazungumzia maslahi mapana ya taifa, na kukataa viashiria vya kusambaratisha nchi hii.
Sio maslahi mapana ya Taifa sema maslahi mapana ya chama . Wenye Taifa hili ni sisi wananchi sio kikundi kichache cha waoga kinachomtetemekea kinyango mlichokichonga wenyewe.
 
Jamaa anatamani aende tena KEZA MBOCHI TOCHA
 
Sikuwa na hamu ya kupiga Kura Ila nitaenda Kwa nguvu zote
 
Akiwa mjini Tunduma, Tundu Lissu katika harakati zake za kutafuta wadhamini, ameongea na maelfu ya wananchi.

Amezungumza kuhusu hali ya uminywaji wa Vyombo vya Habari nchini, watumishi wa umma kutopewa maslahi yao ipasavyo, kero za wafanyabiashara ndogondogo hususan vitambulisho vya wamachinga vya sh 20000, Viongozi wa dini ya waislamu walioko jela kinyume cha haki, uonevu dhidi ya vyama vya siasa, kero ya wafanyabiashara kubambikiziwa kodi na TRA na kusema kuwa watavikomesha hivyo october 28.

Na pia, akampiga kijembe Rais Magufuli kuwa badala ya kuhangaika kuweka bando la internet ili kuwatazama wapinzani kwenye WhatsApp, afungulie vyombo vya habari ili awaone kupitia vyombo rasmi vya habari.

Hapo Tunduma OCD wa sehemu hiyo alijaribu kuwazuia wananchi kwenda mkutanoni, lakini alishindwa kuwathibiti wananchi maana walikuwa ni wengi mno.

Kwa taarifa zaidi muone yeye mwenyewe Tundu Lissu.

Asubiri kampeni ataijua vizuri CCM!
Walivyomuacha, akamaliza maneno yote, risasi zote akafikiri CCM haipo!
CCM ni dola, ni pesa, inamiliki vyote !
 
Mleta mada ni poyoyo....unadhani Rais magufuli anapoteza muda na ka simu mkononi?

Ana vyombo vyake vinampa feeds toka kwenye WhatsApp na mitandao yote.....

Poor argument kusema Rais aweke bando watsapp....kuweka bando hizo ni level za tundu lissu...Rais ni Taasisi ....
 
Me naona hawa majamaa wangekutana wapigane maswali ya live live
 
Chadema ndio waone, hakuna kitu kipya alichokuja nacho lissu. Labda kutumiwa na mabeberu.
Watetezi wa Mabeberu
Walivyofurahia ndege zetu kukamatwa, mikataba mibovu ya madini na serikali kushtakiwa na kufungiwa walikua wanafanya kwa faida ya nani?
 
Hakuna linaloshindikana chini ya jua kinachotakiwa ni umakini katika kushughilika naye, maana ukisikiliza uropokaji wake amekamia kwelikweli ikikibidi hata taifa hili lisambaratike.
why hushughulike nae ali hali kama una uakika uchaguzi utakua fair na atakaeshinda kahalali atangazwe, unafikili kutakua na shida gani? swala hapa sio kushughulika na mtu mmoja swala ni kushughulika na vyama vyote washirika na tume namanisha.
Tume ihakikishe uchaguzi uwe wa haki na halali na alieshida atangazwe , bila kusahau kula kuesabiwa kwa uwazi, na kumtangaza mshindi halali , na hapa sidhani kama kutakua na chama kitaleta shida , sasa wakati tunaangalia vyama vya upinza na misimamo yao kuelekea uchaguzi mkuu lakin hatuangalii na hatujui mpaka sasa msimamo wa chama dola kwamba je watakua tiyari kukubali ikitokea wakashindwa au itakua ni lazima ushindi uwepo na hapo ndo matatizo yanaweza kuanzia,
 
Ni mgombea mmoja Hadi leo anapiga kelele utafikiri Kuna watu amewapa kura wamtunzie!
 
Sio maslahi mapana ya Taifa sema maslahi mapana ya chama . Wenye Taifa hili ni sisi wananchi sio kikundi kichache cha waoga kinachomtetemekea kinyango mlichokichonga wenyewe.

Mwambie huyo kibaraka wa amsterdam hawatapata kitu hapa Tanzania waende DRC huko ndiko wanaendekeza tabia za ushambalabibi.
 
Back
Top Bottom