Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Sabato Njema Wakuu!
Uamuzi wa Mbowe ni sahihi kwa HAKI yake ya kikatiba ila kwa heshima sio uamuzi sahihi. Kwani kushindwa kwake haitakuwa Jambo la kufurahisha na Jambo la heshima. Kustaafishwa kwa kuangukia pua haitakuwa historia nzuri kwa Mhe. Mbowe.
Nina uhakika Lisu atamshinda Mbowe kwa Sababu zifuatazo;
1. Kuondoa uchagadema ndani ya CHADEMA.
Wanachadema wengi hasa wanaotoka kanda zingine hata humu ndani hawafurahishwi na propaganda zinazoendelea kuhusu CHADEMA ni uchagadema.
Kumtoa Mbowe pale kutapunguza hayo madai.
2. Kuondoa kumuabudu mtu.
Kiongozi anapokaa Muda mrefu inajengeka Hali ya kumuogopa, kumuabudu, na yeye kukita mizizi.
Kwa sasa Hapana Shaka Mbowe ni kama mungu mtu hapo CHADEMA. Umungu mtu hutengeneza machawa na worship teams.
3. Wanachadema wengi hawataki kudai HAKI kwa kubembelezana.
Mbowe yeye hupenda kudai HAKI kwa njia ya kumlambalamba mtu miguu. Kumnyenyekea, mazungumzo na njia zote ambazo ni passive.
Kama mjuavyo Njia passive haziletagi matokeo ya haraka. Huweza kuchukua Miaka hata Mia moja. Tofauti na njia active.
CHADEMA wengi wanaamini kwa njia active ambazo Lisu naye huamini hivyo.
Kama CHADEMA ingetumia Njia active kwa kumaanisha Leo hii tungekuwa tunazungumzia habari nyingine hapa. Kariba mpya ingekuwa tayari, hayo mambo ya tume Huru ya uchaguzi yangekuwa mambo madogomadogo kuyashughulikia.
4. Kushindwa kwa Lisu ni kuanguka kwa CHADEMA.
Hilo liko wazi. Wengi wataleta ulinganifu wa sijui wakina Zitto, kina Slaa n.k.
Lakini Lisu lazima ashinde ili CHADEMA iwe hai.
Kwa sasa pale CHADEMA mtu pekee mwenye nafasi ya juu ambaye watu wanaomuona ni mpinzani wa kweli. Yaani anayemaanisha ni Lisu.
Lisu kushindwa ni upinzani kushindwa.
Matokeo ya uchaguzi yataisha Lisu Akiwa mbele kwa 53% Mbowe 46%
Tupumzike