Sera ya majimbo msingi wake ni ubinafsi, ukabila na roho ya uchoyo.
Ni sera ambayo imechukuliwa kutoka nje pasipo kuangalia msingi wa utaifa wetu.
Msingi wa utaifa wa Marekani ni tofauti na ule wa Russia ni tofauti na ule wa Zambia ni tofauti na ule ww Afrika ya Kusini.
Ni sera ambayo ukiitazama kwa juu juu unaweza kudanganyika.
Kwani ukichukuwa Masikini wanne unawaweka kundi moja muujiza gani unatokea!?Usilazimishe Kutokuelewa Kwa Maksudi, unazidi kuudhihirisha ujuha wako.
Je, unayajua Majimbo yatakavyokua na mikoa itakayoyaunda hayo majimbo?
Hiyo singida uisemayo itakua katika jimbo la kati litakalojumuisha mikoa ya MOROGORO, DODOMA SINGIDA NA TABORA. haya hapo umasikini unatokea wapi ikiwa kuna vyanzo vingi vya mapato katk mikoa hiyo.
Mnakera hata kama mnalipwa, wengi ni mambumbumbu. Yaani weupe vichwani.
Mfumo wa Uingereza ni kama wetu tu..US, UK, German, Kenya, South Africa, Nigeria zina majimbo tunazizidi nini.
Vijana watanzania wengi wao yupo wao ni ndogo sana katika masuala ya kimataifaUS, UK, German, Kenya, South Africa, Nigeria zina majimbo tunazizidi nini.
Gharama yake ni kwenye umoja wa kitaifa...madaraka yote kuhodhiwa sehemu moja, na mtu mmoja, ndio uchoyo na ubinafsi.
..lazima wananchi wawe na ngazi ya kiutawala zaidi ya moja inayoweza kutatua shida zao.
..mfumo tulio nao sasa hivi, serikali kuu ikifeli, basi wananchi huko chini hawana namna.
..mfumo wa majimbo utawezesha kuwepo kwa ngazi zaidi ya moja za utawala zinazo-complement one another.
Tunaongelea hatima ya taifa wewe unaleta masuala ya Roman Catholic!!.Kanisa la Roman hapa nchini linaendeshwa kwa mfumo wa majimbo. Mbona haya usemayo hatuyaoni huko?
Gharama yake ni kwenye umoja wa kitaifa.
Pia majimbo maskini hayataweza kuinuliwa tofauti na sasa ambapo pesa ikipatikana inatatua shida kwa mtazamo wa kitaifa.
Barabara zinajengwa kote. Wanafunzi wanasomeshwa kote.
Pesa ya dhahabu ya Shinyanga inasomesha wanafunzi wa vyuo wa nchi nzima.
Pesa ya utalii inagusa wote wa nchi nzima.
Lisu anaongelea tu majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji jimbo litatoa wapi.
Anaeleza kijanja janja huku akificha kuwa uendeshaji jimbo unatakiwa uendeshwe kwa pesa za ndani ya jimbo ikiwemo miradi ya maendeleo.
Chukulia Singida tegemeo lake kuu la uchumi ni kuuza vidumu vya mafuta ya alizeti. Hivyo vyaweza jenga barabara za lami? Kilomita moja tu ya lami inasoma Gharama ya bilioni moja. Hivyo vidumu vya alizeti vyaweza jenga barabara na kulipa mishahara ya wafayakazi wa jimbo?
Afafanue pia kuhusu gharama za kuendesha jimbo asilaghai tu ohh mujiamulie wenyewe.
Ukimsikiliza uaona kabisa mlaghai kwenye gharama za uendeshaji na za miradi ya maendeleo zitakako toka hagusi anahamia hoja nyingine mbio.
Vyovyote unavoweza au penda ita, ila points kuu ni hao viongozi wachaguliwe na wananchi na pia asilimia kubwa ya mapato yatumike pale yalipokusanyiwa kwa wahusika wa jimbo/mkoa kuamua ni nini wanataka kuanza nachoKama tunatumia style iliopo kwa nini unataka majimbo?
Hatujawa tegemezi kwa mtu mmoja mmoja ila huyu mtu hataki tupoteze muda mwingi kwenye siasa za kutoka nje ya bunge wakati bajeti zikiwa zinapitishwa...mbona tulikuwa na umoja wa kitaifa hata wakati majimbo yapo?
..waliovunja mfumo majimbo, pamoja na serikali za mitaa, walilenga kuhodhi madaraka.
..majimbo yalikuwepo na wananchi wa Tanganyika waliungana na kudai uhuru.
..unasema tu kutakuwa na majimbo masikini, hebu tutajie jimbo lenye mikoa ipi litakuwa masikini?
..wanafunzi wanaweza kusoma popote pale nchini, kwa serikali za majimbo kuwa-sponsor, au serikali kuu.
..mimi nawafahamu wazee waliosoma wakati wa mkoloni walipewa msaada na Ma-DC, au walisomeshwa na vyama vya ushirika.
..zaidi itategemea kama tutaamua suala la elimu liwe chini ya majimbo, au serikali kuu. kwa mfano tunaweza kuamua elimu ya sekondari, au ya juu, iwe chini ya mamlaka ya serikali kuu.
..Again, kuna baadhi ya sekta zitaendelea kuwa chini ya serikali kuu. Vilevile serikali kuu itakuwa na jukumu la kusaidia pale ambapo serikali za majimbo zimeshindwa kujimudu.
..Hatuwezi kuendelea kuwa wategemezi na ombaomba kwa mtu mmoja, na mtu mwenyewe anaonyesha ubaguzi na kisarani cha waziwazi. Ni lazima tuweke MFUMO utakaotuweka salama kama taifa.
Next time usini quote kama lengo sio kujibu nilichoulizawakati waukoloni ilikuwa na mikoa ipi?
Hatujawa tegemezi kwa mtu mmoja mmoja ila huyu mtu hataki tupoteze muda mwingi kwenye siasa za kutoka nje ya bunge wakati bajeti zikiwa zinapitishwa.
Hakuna ubaguzi wala kisirani ni ukweli kuwa upinzani unapofanya siasa zinakuwa za kitoto sana.
Magufuli awamu yake imekuwa ikijitahidi kuonyesha uzalendo kwa wananchi lakini tunapenda mno siasa za midomoni ambazo mataifa makin yamesha achana nazo.
Majimbo maskini ni kina Singida, Dodoma na hata kule Katavi na Rukwa kukiachwa kwa visingizio vya majimbo kutabaki nyuma kwa miaka mingi ijayo.
Tunaongelea hatima ya taifa wewe unaleta masuala ya Roman Catholic!!.
Uchoyo utatoka wapi?
Mbona nyie kwa mfumo wa sasa ndo mnafanya uchoyo na ubaguzi? Kwa nini Magufuli alisema hawezi kujenga stand jimboni kwa mbunge Bwege kwa sababu ni mpinzani?
Kwa ini Magufuli amesema wazi mchana kweupe kwenye kampeni zake kuwa hawezi peleka maendeleo sehemu watakazochagua wapinzani?