..mbona tulikuwa na umoja wa kitaifa hata wakati majimbo yapo?
..waliovunja mfumo majimbo, pamoja na serikali za mitaa, walilenga kuhodhi madaraka.
..majimbo yalikuwepo na wananchi wa Tanganyika waliungana na kudai uhuru.
..unasema tu kutakuwa na majimbo masikini, hebu tutajie jimbo lenye mikoa ipi litakuwa masikini?
..wanafunzi wanaweza kusoma popote pale nchini, kwa serikali za majimbo kuwa-sponsor, au serikali kuu.
..mimi nawafahamu wazee waliosoma wakati wa mkoloni walipewa msaada na Ma-DC, au walisomeshwa na vyama vya ushirika.
..zaidi itategemea kama tutaamua suala la elimu liwe chini ya majimbo, au serikali kuu. kwa mfano tunaweza kuamua elimu ya sekondari, au ya juu, iwe chini ya mamlaka ya serikali kuu.
..Again, kuna baadhi ya sekta zitaendelea kuwa chini ya serikali kuu. Vilevile serikali kuu itakuwa na jukumu la kusaidia pale ambapo serikali za majimbo zimeshindwa kujimudu.
..Hatuwezi kuendelea kuwa wategemezi na ombaomba kwa mtu mmoja, na mtu mwenyewe anaonyesha ubaguzi na kisarani cha waziwazi. Ni lazima tuweke MFUMO utakaotuweka salama kama taifa.