Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

Sera ya majimbo msingi wake ni ubinafsi, ukabila na roho ya uchoyo.

Ni sera ambayo imechukuliwa kutoka nje pasipo kuangalia msingi wa utaifa wetu.

Msingi wa utaifa wa Marekani ni tofauti na ule wa Russia ni tofauti na ule wa Zambia ni tofauti na ule ww Afrika ya Kusini.

Ni sera ambayo ukiitazama kwa juu juu unaweza kudanganyika.

Kanisa la Roman hapa nchini linaendeshwa kwa mfumo wa majimbo. Mbona haya usemayo hatuyaoni huko?
 
Wanacdm nawaonya nimechelewa kuwatahadharisha, sera za cdm ndo maccm wanatekeleza, kwa hiyo mkitoa elimu jinsi ya kuendesha serikali za majimbo mtakuwa mmewapa somo na muda si mrefu watatekeleza, mwisho wa safari cdm itakuwa haina sera za kutembelea. Wenye akili mmenielewa
 
Usilazimishe Kutokuelewa Kwa Maksudi, unazidi kuudhihirisha ujuha wako.

Je, unayajua Majimbo yatakavyokua na mikoa itakayoyaunda hayo majimbo?

Hiyo singida uisemayo itakua katika jimbo la kati litakalojumuisha mikoa ya MOROGORO, DODOMA SINGIDA NA TABORA. haya hapo umasikini unatokea wapi ikiwa kuna vyanzo vingi vya mapato katk mikoa hiyo.

Mnakera hata kama mnalipwa, wengi ni mambumbumbu. Yaani weupe vichwani.
Kwani ukichukuwa Masikini wanne unawaweka kundi moja muujiza gani unatokea!?

1) Shida zao zinakuwa chache au wote wanakuja na shida zao zile zile walizokuwa nazo wakiwa nje ya jumuiko!?

2) rasilimali zao zinaongezeka au inakuwa tu jumla ya rasilima zao chache na ndogo walizokuwa nazo kabla ya kuungana!?

Ukweli ni kuwa serikali za kijimbo zina hasara zaidi ya faida..

Zitachochea mpasuko wa kitaifa.. kwani wazawa wa kagera watataka rasilimali zao ziwanufaishe wao pekee

Ajira zitategemea uwezo wa jimbo kuzalisha na ukiangalia majimbo masikini ndiyo yenye watu wengi pia sijui hili Mh. Adv. Lissu Amelizingatia.

Umoja wa kitaifa uliopo unachagizwa na kutokuwepo serikali za kijimbo, leo mhehe anaendesha mkoa wa kigoma na muha anaendesha Kilimanjaro.

Mkaguru ni mkurugenzi mwanza na msukuma ni afisa maendeleo mpanda. Tunapokosa dawa Singida kodi za Mbeya zinacover na tupopigwa na baa la njaa Shinyanga mahindi ya Iringa yanatuokoa.

This balance is genius. Unless kuwe na aina tofauti ya jimbo lakini nadhani tuko kwenye njia salama kabisa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
US, UK, German, Kenya, South Africa, Nigeria zina majimbo tunazizidi nini.
Mfumo wa Uingereza ni kama wetu tu..
Wana states kama sisi tulivyo na Zanzibar na Tanzania bara.. na ndani ya kila states(Jimbo) wana mikoa na miji.

USA yenyewe utofauti wake na sisi ni kuwa kile kilichotokea kati yetu na Zanzibar kilitokea in a much larger scale. States zote zilikuwa functional na zikiwa na uwezo wa kiuchumi na kujiendesha hivyo ziliingia chini ya mwamvuli wa USA zikiwa na matakwa yao pia...

Utofauti na Tanzania Bara hakukuwa na organised communities ambazo zilikuwa serikali thabiti na uwezo wa kujiendesha ili zidai kuwa tu chini ya umoja wa Tanzania kama ilivyo kwa Zanzibar lakini zijiendeshe zenyewe kwa mambo ya ndani.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
..madaraka yote kuhodhiwa sehemu moja, na mtu mmoja, ndio uchoyo na ubinafsi.

..lazima wananchi wawe na ngazi ya kiutawala zaidi ya moja inayoweza kutatua shida zao.

..mfumo tulio nao sasa hivi, serikali kuu ikifeli, basi wananchi huko chini hawana namna.

..mfumo wa majimbo utawezesha kuwepo kwa ngazi zaidi ya moja za utawala zinazo-complement one another.
Gharama yake ni kwenye umoja wa kitaifa.

Pia majimbo maskini hayataweza kuinuliwa tofauti na sasa ambapo pesa ikipatikana inatatua shida kwa mtazamo wa kitaifa.

Barabara zinajengwa kote. Wanafunzi wanasomeshwa kote.

Pesa ya dhahabu ya Shinyanga inasomesha wanafunzi wa vyuo wa nchi nzima.

Pesa ya utalii inagusa wote wa nchi nzima.
 
..mbona tulikuwa na umoja wa kitaifa hata wakati majimbo yapo?

..waliovunja mfumo majimbo, pamoja na serikali za mitaa, walilenga kuhodhi madaraka.

..majimbo yalikuwepo na wananchi wa Tanganyika waliungana na kudai uhuru.

..unasema tu kutakuwa na majimbo masikini, hebu tutajie jimbo lenye mikoa ipi litakuwa masikini?

..wanafunzi wanaweza kusoma popote pale nchini, kwa serikali za majimbo kuwa-sponsor, au serikali kuu.

..mimi nawafahamu wazee waliosoma wakati wa mkoloni walipewa msaada na Ma-DC, au walisomeshwa na vyama vya ushirika.

..zaidi itategemea kama tutaamua suala la elimu liwe chini ya majimbo, au serikali kuu. kwa mfano tunaweza kuamua elimu ya sekondari, au ya juu, iwe chini ya mamlaka ya serikali kuu.

..Again, kuna baadhi ya sekta zitaendelea kuwa chini ya serikali kuu. Vilevile serikali kuu itakuwa na jukumu la kusaidia pale ambapo serikali za majimbo zimeshindwa kujimudu.

..Hatuwezi kuendelea kuwa wategemezi na ombaomba kwa mtu mmoja, na mtu mwenyewe anaonyesha ubaguzi na kisarani cha waziwazi. Ni lazima tuweke MFUMO utakaotuweka salama kama taifa.
 
Lisu anaongelea tu majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji jimbo litatoa wapi.

Anaeleza kijanja janja huku akificha kuwa uendeshaji jimbo unatakiwa uendeshwe kwa pesa za ndani ya jimbo ikiwemo miradi ya maendeleo.

Chukulia Singida tegemeo lake kuu la uchumi ni kuuza vidumu vya mafuta ya alizeti. Hivyo vyaweza jenga barabara za lami? Kilomita moja tu ya lami inasoma Gharama ya bilioni moja. Hivyo vidumu vya alizeti vyaweza jenga barabara na kulipa mishahara ya wafayakazi wa jimbo?

Afafanue pia kuhusu gharama za kuendesha jimbo asilaghai tu ohh mujiamulie wenyewe.

Ukimsikiliza uaona kabisa mlaghai kwenye gharama za uendeshaji na za miradi ya maendeleo zitakako toka hagusi anahamia hoja nyingine mbio.

Kwa akili yako umemsikia akisema Singida ni jimbo?
Huoni kuwa anataka kuondoa hii dhana mfu ya kimkoa ambayo inaziangamizima mikoa yenye changamoto za fursa pana?
Acha kupotosha. Unapotosha kwa masilahi ya nani?
Hivi watanzania mna nini?
 
Ulitaka aseme kila kitu kwenye kampeni?
 
Kama tunatumia style iliopo kwa nini unataka majimbo?
Vyovyote unavoweza au penda ita, ila points kuu ni hao viongozi wachaguliwe na wananchi na pia asilimia kubwa ya mapato yatumike pale yalipokusanyiwa kwa wahusika wa jimbo/mkoa kuamua ni nini wanataka kuanza nacho
 
..mbona tulikuwa na umoja wa kitaifa hata wakati majimbo yapo?

..waliovunja mfumo majimbo, pamoja na serikali za mitaa, walilenga kuhodhi madaraka.

..majimbo yalikuwepo na wananchi wa Tanganyika waliungana na kudai uhuru.

..unasema tu kutakuwa na majimbo masikini, hebu tutajie jimbo lenye mikoa ipi litakuwa masikini?

..wanafunzi wanaweza kusoma popote pale nchini, kwa serikali za majimbo kuwa-sponsor, au serikali kuu.

..mimi nawafahamu wazee waliosoma wakati wa mkoloni walipewa msaada na Ma-DC, au walisomeshwa na vyama vya ushirika.

..zaidi itategemea kama tutaamua suala la elimu liwe chini ya majimbo, au serikali kuu. kwa mfano tunaweza kuamua elimu ya sekondari, au ya juu, iwe chini ya mamlaka ya serikali kuu.

..Again, kuna baadhi ya sekta zitaendelea kuwa chini ya serikali kuu. Vilevile serikali kuu itakuwa na jukumu la kusaidia pale ambapo serikali za majimbo zimeshindwa kujimudu.

..Hatuwezi kuendelea kuwa wategemezi na ombaomba kwa mtu mmoja, na mtu mwenyewe anaonyesha ubaguzi na kisarani cha waziwazi. Ni lazima tuweke MFUMO utakaotuweka salama kama taifa.
Hatujawa tegemezi kwa mtu mmoja mmoja ila huyu mtu hataki tupoteze muda mwingi kwenye siasa za kutoka nje ya bunge wakati bajeti zikiwa zinapitishwa.

Hakuna ubaguzi wala kisirani ni ukweli kuwa upinzani unapofanya siasa zinakuwa za kitoto sana.

Magufuli awamu yake imekuwa ikijitahidi kuonyesha uzalendo kwa wananchi lakini tunapenda mno siasa za midomoni ambazo mataifa makin yamesha achana nazo.

Majimbo maskini ni kina Singida, Dodoma na hata kule Katavi na Rukwa kukiachwa kwa visingizio vya majimbo kutabaki nyuma kwa miaka mingi ijayo.
 
Navyoona ni uelewa tu.kuwa na serikali za majimbo haimaanishi kuwa hakuna serikali ya kitaifa. Navyojua kunakua na federal government ambayo yenyewe inasimamia projects za kitaifa bila kuangalia majimbo. Ni suala la uelewa tuu.
 
Kichaa sio lazima avue nguo kwani hela kuendesha mikoa zinatoka wapi? Kwani serikali zenye majimbo kote duniani zinajiendeshaje?
 
Hatujawa tegemezi kwa mtu mmoja mmoja ila huyu mtu hataki tupoteze muda mwingi kwenye siasa za kutoka nje ya bunge wakati bajeti zikiwa zinapitishwa.

Hakuna ubaguzi wala kisirani ni ukweli kuwa upinzani unapofanya siasa zinakuwa za kitoto sana.

Magufuli awamu yake imekuwa ikijitahidi kuonyesha uzalendo kwa wananchi lakini tunapenda mno siasa za midomoni ambazo mataifa makin yamesha achana nazo.

Majimbo maskini ni kina Singida, Dodoma na hata kule Katavi na Rukwa kukiachwa kwa visingizio vya majimbo kutabaki nyuma kwa miaka mingi ijayo.

..Umesahau majuzi Jpm alisema maeneo yanayochagua wabunge toka vyama vya upinzani hayatapewa fedha za miradi ya maendeleo?

..sasa ili wananchi wawe na "bima" ya kuwakinga dhidi ya viongozi wabaguzi ni afadhali tuwe na mfumo wa utawala ambao madaraka hayatahodhiwa ktk ngazi moja, chini ya mtu mmoja.
 
"Mbona nyie kwa mfumo wa sasa ndo mnafanya uchoyo na ubaguzi? Kwa nini Magufuli alisema hawezi kujenga stand jimboni kwa mbunge Bwege kwa sababu ni mpinzani?"

Mkuu hiko ulichosema ndo Tundu Lissu anataka kuwe na serikali ya wananchi vitu kama hivyo vinamalizwa na mkoa wenyewe sio mpaka wamlambe miguu Rais kama sasa Rais anafanywa Mungu kila kitu ni yeye.
Uchoyo utatoka wapi?

Mbona nyie kwa mfumo wa sasa ndo mnafanya uchoyo na ubaguzi? Kwa nini Magufuli alisema hawezi kujenga stand jimboni kwa mbunge Bwege kwa sababu ni mpinzani?

Kwa ini Magufuli amesema wazi mchana kweupe kwenye kampeni zake kuwa hawezi peleka maendeleo sehemu watakazochagua wapinzani?
 
Back
Top Bottom